Chama cha Soka cha Spain, RFEF, kimempa
Mchezaji huyo wa Real Madrid ambae pia ndio Mchezaji Bora Duniani
Kifungo cha Mechi 3 kufuatia Kadi Nyekundu aliyopewa kwenye Mechi na
Athletic Bilbao Jumapili iliyopita ambayo ilimalizika kwa Sare ya Bao
1-1.
Ronaldo, ambae Leo anasheherekea Miaka
29 tangu kuzaliwa, alipewa Kadi Nyekundu kwenye Dakika ya 76 baada
kukwaana na Wachezaji wa Bilbao Ander Iturraspe na Carlos Gurpegui.
RFEF imempa Ronaldo Kifungo cha Mechi
moja kufuatia Kadi Nyekundu na kumuongezea Mechi mbili kwa kutoa ishara
iliyotafsiriwa kuwa ni kebehi kwa Marefa wakati akitoka nje mara baada
ya Kadi hiyo.
Kifungo hiki cha Mechi tatu kinamaanisha
atazikosa Mechi za Real Madrid za La Liga dhidi ya Villareal, Februari
9, na Elche, Februari 23, zote zitachezwa Uwanjani Santiago Bernabeu na
ile ya Ugenini hapo Februari 16 na Getafe.
Licha ya Kifungo hiki, Ronaldo yuko huru
kuichezea Real Mechi zote mbili za Nusu Fainali ya Copa del Rey dhidi
ya Atletico Madrid ambayo ya Kwanza ni Leo na Marudiano ni Wiki ijayo.
0 comments:
Post a Comment