Thursday, 20 February 2014

ARGENTINA: MESSI, AGUERO NDANI, CARLOS TEVEZ NJE!

>>SASA NAFASI YA TEVEZ KWENDA BRAZIL FINYU!!

MESSI_IN_ARGENTINAKWA MARA NYINGINE tena Straika wa Juventus, Carlos Tevez, hakuchuliwa kwenye Kikosi cha Argentina na hii inaashiria nafasi yake kuichezea Nchi yake huko Brazil kwenye Fainali za Kombe la Dunia ni finyu kama hamna kabisa.TEVEZ_IN_JUVE
Kocha wa Argentina, Alejandro Sabella, ameteua Kikosi chake cha Wachezaji 22 kuwavaa Romania hapo Machi 5 huko Bucharest na kama ilivyo kawaida yake tangu awe Kocha wa Nchi hiyo Tevez hakuitwa.
Msimu huu akiwa na Juventus, Carlos ameshafunga Bao 14 na mara ya mwisho kuichezea Argentina ni kwenye Copa America Mwaka 2011 wakati Kocha wa Argentina ni Sergio Batista.
Wachezaji wengine maarufu ambae hawakuitwa ni Esteban Cambiasso, Kipa wa Malaga, Willy Caballero, na Fowadi wa Tottenham, Erik Lamela.
Kikosini, kama ilivyotarajiwa na wengi, wamo Mafowadi hatari, Lionell Messi na Sergio Aguero.
Baada ya kucheza na Romania, Argentina watacheza Mechi nyingine za Kirafiki dhidi ya Trinidad & Tobago na Slovenia Mwezi Juni.
Kwenye Fainali za Kombe la Dunia huko Brazil, Argentina wako Kundi F pamoja na Bosnia-Herzegovina, Iran na Nigeria.
KIKOSI KILICHOTEULIWA:
Makipa: Sergio Romero (Monaco), Mariano Andujar (Catania)
Mabeki: Pablo Zabaleta (Manchester City), Federico Fernandez (Napoli), Ezequiel Garay (Benfica), Marcos Rojo (Sporting Lisbon), Hugo Campagnaro (Inter), Jose Basanta (Monterrey), Lisandro Lopez (Getafe), Nicolas Otamendi (Atletico Mineiro), Gino Peruzzi (Catania)
Viungo: Javier Mascherano (Barcelona), Angel Di Maria (Real Madrid), Lucas Biglia (Lazio), Ricardo Alvarez (Inter), Augusto Fernandez (Celta Vigo), Jose Sosa (Atletico Madrid)
Mafowadi: Lionel Messi (Barcelona), Gonzalo Higuain (Napoli), Sergio Aguero (Manchester City), Ezequiel Lavezzi (Paris Saint-Germain), Rodrigo Palacio (Inter).

Related Posts:

0 comments: