Thursday, 9 January 2014

ZITTO KABWE ASEMA YEYE HATAKI MALUMBANO

        Zitto: Sitaki malumbano

*Asema ni muda wa kutumikia wapiga kura, kuibana Serikali
Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe
MBUNGE wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe (CHADEMA), amesema kuanzia sasa hataki malumbano na mtu. Kauli ya Zitto, imekuja siku moja baada ya Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, kupiga marufuku chombo chochote kujadili uanachama wake. Akizungumza na MTANZANIA mjini Dar es Salaam jana, Zitto alisema ameamua kukaa kimya ili kupata muda mzuri wa kutafakari misukosuko ya kisiasa aliyokumbana nayo.

“Kuanzia sasa naomba kukwambia sitaki malumbano na mtu, natafakari misukosuko ya kisiasa niliyokumbana nayo kwanza,” alisema Zitto.

Alisema hayuko tayari kujibizana na mtu yeyote na kwamba anataendelea kufanya kazi ya kuwawakilisha wananchi wa jimbo lake.

Alisema jukumu jingine lililo mbele yake ni kutunga sheria ndani ya Bunge na kuisimamia Serikali kupitia Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC).


Chanzo mtanzania
 Na Bakari Kimwanga, Dar es Saalm

Related Posts:

0 comments: