>> JIJINI DAR: LEO SIMBA v MTIBWA, UWANJA WA TAIFA, KIINGILIO BUKU 5!
SOMA ZAIDI:
ZIARA YANGA-TURKEY: LEO NA KS FLAMURTARI VLORE YA ALBANIA!
Mechi hii, ikiwa ni ya tatu kwa Yanga
kucheza huko Uturuki ambako iko kwa Ziara ya Wiki 2 ya Mazoezi,
itachezwa huko Side Manavagat Mjini Antalya na ni dhidi ya Klabu Kongwe
kutoka Nchi ya Albania, KS Flamurtari Vlore, ambayo inacheza Ligi Kuu
Albania na Msimu huu inakamata Nafasi ya 5.
Katika Mechi mbili za kujipima nguvu huko Nchini Uturuki, Yanga ilizifunga Ankara Sekerspor Bao 3-0 na 2-0 Altay SK Bao 2-0.
Kwa sasa Yanga iko chini ya Kocha wao
mpya, Hans Van Der Plyum, kutoka Uholanzi ambae alijiunga na Timu huko
Uturuki mapema Wiki hii na anasaidiwa na Makocha Charles Boniface Mkwasa
na Juma Pondamali.
Kabla ya kurejea Dar es Salaam Wiki
ijayo, Yanga inatarajiwa kucheza Mechi nyingine ya kujipima nguvu na
Simurq PIK inayoshikri Ligi Kuu nchini Azerbaijan.
JIJINI DAR: LEO SIMBA v MTIBWA, UWANJA WA TAIFA
Simba leo itacheza Mechi ya Kirafiki na Mtibwa Sugar Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.
Kiingilio kwa Mechi hii itakayoanza Saa 10 Jioni ni Shilingi 5,000.
0 comments:
Post a Comment