>>KOCHA MHOLANZI AANZA VYEMA!
>>SIMBA JUMAMOSI TAIFA NA MTIBWA SUGAR!
>>TFF YATOA RAMBIRAMBI MSIBA WA MWAMUZI MSEBULA
SOMA ZAIDI:
MABINGWA YANGA, ambao wamepiga Kambi huko Antalya, Uturuki, leo wamecheza Mechi yao ya
Pili
ya kujipima nguvu na kuichapa Klabu ya Daraja la Pili ya Nchini humo,
Altay SK, Bao 2-0 kwenye Mechi iliyochezwa Viwanja vya Sueno.
Katika Mechi ya Kwanza hapo Juzi, Yanga iliichapa Ankara Sekerspor Bao 3-0.
Hii leo, Yanga ilikuwa na Kocha wao mpya
kutoka Uholanzi, Hans Van Der Plyum, na ilishinda kwa Bao za Didier
Kavumbagu, Dakika ya 46, na Emmanuel Okwi, Dakika ya 57.
Hans Van Der Plyum-Klabu alizofundisha:
-Medeama SC [Ghana]: 16.07.2013 hadi 24.10.2013
-Berekum Chelsea [Ghana]: 01.11.2011 hadi 16.07.2013
-Heart of Lions Kpando [Ghana]: 01.07.2010 hadi 20.09.2011
-Ashanti Gold SC [Ghana]: 01.07.2004 hadi 05.10.2005
-Heart of Lions Kpando [Ghana]: 01.07.2002 hadi 20.07.2003
-Ashanti Gold SC [Ghana]: 01.07.2000) hadi 30.06.2002
-Excelsior Rotterdam [Holland]: 01.07.1995 hadi 30.06.1996
-FC Den Bosch [Holland]: 01.07.1990) hadi 30.06.1995
Yanga, ambayo itakuwa Uturuki kwa Wiki mbili, inatarajiwa kucheza Mechi yake ya Tatu huko Uturuli hivi karibuni.
KIKOSI CHA YANGA HII LEO:
Ally Mustafa "Barthez", Juma Abdul,
Oscar Joshua, Mbuyu Twite, Kelvin Yondani, Frank Domayo, Haruna
Niyonzima, Hassan Dilunga, Didier Kavumbagu, Mrisho Ngasa, Emmanuel Okwi
Akiba: Juma Kaseja, David Luhende, Ibrahim Job, Nizar Khalfan, Hamis Kizza, Jerson Tegete, Saimon Msuva
SIMBA NA MTIBWA SUGAR, JUMAMOSI, UWANJA WA TAIFA
Wakati Watani zao wakivinjari huko
Majuu, Simba wao wamerudi Dar es Salaam baada Juzi kuchapwa Bao 1-0 na
KCC kwenye Fainali ya Mapinduzi Cup na Jumamosi hii watatua Uwanja wa
Taifa Jijini Dar es Salaam kujipima nguvu na Mtibwa Sugar.
TOKA TFF:
Release No. 007
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Januari 15, 2014
RAMBIRAMBI MSIBA WA MWAMUZI MSEBULA
Shrikisho la Mpira wa Miguu Tanzania
(TFF) limepokea kwa masikitiko kifo cha mwamuzi Methusela Msebula
kilichotokea juzi (Januari 13 mwaka huu) katika Wilaya ya Bukombe mkoani
Geita.
Mwamuzi Msebula ambaye alikuwa mwamuzi
daraja la kwanza (class one) alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa
kisukari, maradhi ambayo yalimsababisha kuwa nje ya uchezeshaji mechi za
mpira wa miguu kwa karibu misimu miwili.
Msiba huu ni mkubwa kwa jamii ya mpira
wa miguu kwani, Msebula alitoa mchango mkubwa katika fani ya uamuzi
nchini, hivyo mchango wake tutaukumbuka daima. Marehemu anatarajiwa
kuzikwa leo (Januari 15 mwaka huu) nyumbani kwao Kanyigo, Bukoba mkoani
Kagera.
TFF tunatoa pole kwa familia ya marehemu
Msebula, Chama cha Waamuzi wa Mpira wa Miguu Tanzania (FRAT) na Chama
cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Geita (GEREFA) na kuwataka kuwa na subira na
uvumilivu katika kipindi hiki kigumu cha msiba huo mzito.
Bwana alitoa, Bwana ametwaa jina lake lihimidiwe. Amina
Boniface Wambura Mgoyo
Ofisa Habari na Mawasiliano
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
0 comments:
Post a Comment