Meneja wa Mamlaka ya Mapato Nchini (TRA) Makao Mkuu, Gabriel Mwangosi akitoa mada wakati wa semina ya kodi kwa viongozi wa taasisi mbalimbali za dini nchini iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), imenunua mashine 8,000 za kutolea risiti za kieletroniki (EFD), ambazo zitagawiwa kwa wafanyabiashara wadogo wadogo nchini.
Meneja wa masuala ya Kodi (TRA), Gabriel Mwangosi, aliyasema hayo jijini Dar es Salaam jana alipohojiwa kuhusu utekelezaji wa agizo la Rais John Magufuli, kwamba wafanyabiasha wagawiwe bure mashine hizo.
Alisema kuwa mashine hizo ni kati ya 200,000 ambazo TRA imeweka mkakati wa kuzigawa bure kwa wafanyabiasha, ili kudhibiti ukwepaji kodi na kukuza mapato.
Awali akifungua semina kwa Chama cha Walimu wenye Ulemavu (CWUT), Mwangosi alisema mafunzo hayo yamelenga kuwapa elimu watu walio katika makundi maalum pamoja na Watanzania kwa ujumla, ili kufahamu umuhimu wa kulipa kodi.
“Lengo ni kukusanya kodi, uwe umeajiriwa, mfanyabiashara ni wajibu kulipa kodi kutokana na kile ambacho unakipata. Kuna kodi za aina mbalimbali ambazo zinalipwa na tutaendelea kutoa mafunzo nchi nzima,” alisema Mwangosi.
Mmoja wa washiriki wa mafunzo hayo, Fransis Mbisso, mwalimu wa Shule ya Sekondari Zanaki, alisema mafunzo hayo yamemwongezea elimu juu ya umuhimu wa kulipa kodi pamoja na kupatiwa risiti katika kila huduma na bidhaa anayoipata.
“Watanzania tulio wengi hatuna utaratbu wa kudai risiti bada ya kununua kitu au kupatiwa huduma Fulani. Ni haki ya mnunuzi na hiyo inatoa kumbukumbu ya kulipa kodi kwa mfanyabiashara,” alisema Mbisso.
0 comments:
Post a Comment