Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi ameiagiza bodi ya Shirika la Nyumba la Taifa Nyumba (NHC) kuacha kuanzisha miradi mipya ya ujenzi hadi kukamilishwa kwa miradi iliyokwishaanza.
Akizungumza na wajumbe wa bodi hiyo Dar es Salaam jana, Lukuvi alisema hakuna haja ya kuanzisha miradi mipya wakati iliyopo haijakamilika.
“Nadhani miradi iliyopo mnaijua na tarehe za kukamilika ujenzi wake wote tunafahamu, hivyo nitoe agizo kuanzia leo hakuna kuanza kwa mradi mpya wowote mpaka imalizwe iliyokwishaanza,” alisema.
Lukuvi pia aliiagiza bodi hiyo kutopandisha kodi za nyumba zake bila ridhaa yake huku akisisitiza gharama zipangwe kwa kuzingatia uwezo wa wananchi.
“Hamuwezi kusema nyumba ya gharama nafuu wakati ina vyumba viwili na inauzwa kwa Sh52 milioni, hainiingii akilini na wala Mtanzania wa kawaida hawezi kuona unafuu wowote hapo,” alisema Lukuvi.
0 comments:
Post a Comment