Baada ya uwanja wa Mkwakwani kutajwa kuwa mgumu msimu huu kupata matokeo kwaYanga na Azam FC, March 19 ilikuwa ni zamu ya wekundu wa Msimbazi Simbakupambana na Coastal Union ambapo kwa Yanga na Azam FC zote ziliambulia kipigo cha goli 1-0 dhidi ya Coastal Union.
Simba walikuwa wanatizamiwa kupata wakati mgumu kama walikokuwa wameupataYanga na Azam FC, kitu ambacho kiliwafanya waanze mchezo kwa umakini mkubwa,Coastal walionesha jitihada kiasi, lakini juhudi za Simba zilizaa matunda dakika ya 39 baada ya Danny Lyanga kupachika goli la uongozi kwa Simba.
Kipindi cha kilimalizika kwa Simba kwenda mapumziko wakiwa mbele kwa goli 1-0, goli ambalo lilikuwa chachu ya wao kuendelea kufanya vizuri katika mchezo huo, kipindi cha pili dakika ya 51 Hamis Kiiza alitumia vizuri krosi ya Emily Nimubona na kupiga kichwa kilichozaa goli la pili.
Hadi dakika 90 zinamalizika Simba walifanikiwa kuibuka na ushindi wa goli 2-0 na kupata point tatu, kwa matokeo hayo Simba anaendelea kuongoza Ligi kwa jumla ya point 57 akiwa kacheza michezo 24, lakini kawazidi Yanga na Azam FC point saba na michezo mitatu.
0 comments:
Post a Comment