Siku ya Figo duniani, ni tukio la kimaarifa na la kuleta mwangaza duniani linaloadhimishwa mwezi Machi. Kila mwaka, kumekuwepo na shughuli mbalimbali kitaifa na kimataifa zinazofanywa na mashirika mbalimbali ya Figo, mahospitali, wataalamu wa afya na watu binafsi wanaotaka kuleta mabadiliko duniani dhidi ya ugonjwa wa figo. Ni muhimu kuhimiza elimu, vipimo vya awali, na mtindo mzuri wa maisha ili kuruhusu Jamii itambue magonjwa ya Figo yanayoathiri watu milioni duniani ikiwemo watoto ambao wapo katika hatari ya kuugua katika umri mdogo. Kampeni ya mwaka 2016 ina lengo mahususi kwa magonjwa ya Figo na watoto.
Matatizo ya figo kwa watoto yajulikanayo kitaalamu kama (Paediatric Nephology aliments) yanahusiana na magonjwa ya Figo kwa watoto wachanga na watoto wadogo mpaka miaka kumi na nane. Kwa mujibu wa Dk. Mehul A. Shah, Mtaalamu wa magonjwa ya figo kwa watoto kutoka Hospitali za Apollo; Hyderabad Magonjwa ya Figo kwa watoto yanaweza tokea Sababu ya mapungufu katika ukuaji au maumbile (yanayotokea wakati wa kujifungua), kurithi (katika familia) au mabadiliko katika mazingira/ kinga mwilini au madawa. Matatizo Kama hayo yakitambulika mapema huweza zuia uharibifu wa Figo.
Dk. Shah anawahimiza watanzania kufwata mbinu za kuzuia matatizo ya Figo kwa watoto ambazo zitasaidia kujenga Tanzania isio na magonjwa ya Figo. Mbinu izi ni kama Kupima mkojo kwa watoto wadogo chini ya umri wa miaka miwili wenye homa kali, kuhimiza watoto wasiozidi miaka mitatu kukojo kwa wakati (wasibane mkojo), ulaji wa matunda na mbogamboga, chumvi ya kiasi na nyama katika milo ya familia.
Dk. Mehul A. Shah, Mtaalamu wa magonjwa ya figo kwa watoto kutoka Hospitali za Apollo; Hyderabad akitoa huduma kwa mtoto.
Kupunguza muda unaotumika na watoto katika televesheni na kompyuta na kuongeza shughuli nyingi Zaidi zenye kupunguza ongezeko la uzito, kuepuka dawa za kupunguza maumivu kama Nimesulide, Ibuprofen n.k. pamoja na madawa ya Ayurvedic/Unani, matumizi ya Crocin/ Calpol/ Paracetamol, kupima presha angalau mara moja kwa mwaka kwa watoto wenye Zaidi ya miaka mitatu, kufanya uchunguzi wa ugonjwa wa Figo kwa mtoto mwenye matatizo katika ukuaji, anemia, shinikizo la damu, damu katika mkojo, kuvimba kwa mwili au maambukizi ya mkojo ya mara kwa mara. Mbinu hizi pia zimetajwa na Dk. Shah kama njia za kuepuka magonjwa ya Figo kwa Watoto.
Matatizo ya Figo yanaweza tokea kwa watoto kutokana na matatizo katika maumbile au yanayotokea baada ya kuzaliwa. Wataalamu wa magonjwa ya figo kwa watoto kutoka Hospitali za Apollo wanahimiza upimaji wa mara kwa mara ili kufahamu kama mtoto wako ana matatizo ya figo.
0 comments:
Post a Comment