Mwenyekiti wa Serikali ya kijiji cha Makibo Wilayani Sikonge Mkoani Tabora, Petro Ntakulo, ameuawa kwa kuchomwa na moto na kundi la watu wasiojulikana kisha kutokomea kusikojulikana.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Hamis Issah alisema tukio hilo limetokea usiku katika kijiji hicho kilichopo kata ya Nyahua.
Akielezea tukio hilo, alisema kulitokea sintofahamu iliyosababisha watu kukusanyika kufahamu kilichotokea na ndipo watu wasiojulikana wakamvamia mwenyekiti huyo na kumkata mapanga na kuuchoma mwili wake kwa moto.
Kamanda Issa alisema chanzo cha tukio hilo bado hakijajulikana ambapo Jeshi hilo kwa kushirikiana na wananchi wanazidi kufanya uchunguzi ili kuweza kubaini chanzo cha mauaji hayo.
Kwa mujibu wa mmoja wa wakazi wa eneo hilo,Daud Musa, mbali ya kufanya mauaji hayo,watu hao pia walibomoa nyumba za marehemu na kuchoma mali zake .
Alizidi kueleza kuwa watu hao walikuwa wakidai kuwa hawataki kuwaona viongozi wa serikali eneo lao na kwamba hata wazee nao hawatakiwi.
Alieleza kuwa ulipigwa mwano (ishara ya hatari) na wananchi kukusanyika na ndipo baadhi yao waliokuwa wamejiandaa kufanya mauaji kutekeleza malengo yao.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Peter Nzalalila, amewataka wananchi kuacha kujichukulia sheria mkonono na badala yake wafuate sheria kwani kufanya hivyo ni kuvunja sheria za nchi.
Tukio hilo limeacha simanzi kubwa kwa wakazi wa eneo hilo, wakisema marehemu alikuwa kiongozi mzuri na aliyejua wajibu wake.

"Wananchi wanapaswa kutii mamlaka zilizopo na sio kujichukulia sheria mkononi bali waache vyombo vya dola vifanye kazi yake’’ alisema Nzalalila.
Tukio hilo limeacha simanzi kubwa kwa wakazi wa eneo hilo, wakisema marehemu alikuwa kiongozi mzuri na aliyejua wajibu wake.
0 comments:
Post a Comment