Msanii wa bongo fleva nchini Linah Sanga amefunguka na kusema kuwa alikuwa anatamani na bado anatamani sana kuwa na mahusiano ya kimapenzi na msanii Wizkid kutoka nchini Nigeria.
Akipiga stori kwenye kipindi cha eNEWS kinachorushwa na ting’a namba moja kwa vijana (EATV) Linah Sanga alisema kuwa toka kipindi cha nyuma alikuwa anatamani kuwa na msanii huyo kama mpenzi wake, ingawa anadai mpaka sasa ndoto yake hiyo haijaweza kukamilika mpaka dakika hii.
“Unajua nilikuwa namu admire Wizkid toka muda mrefu, na ndiyo mwanaume ambaye hata ukiniuliza ni msanii gani wa kiume katika bara la Afrika ambaye ungependa kuwa naye au ambaye nampenda nitakwambia ni Wizkid, siwezi kukataa ila ndiyo hivyo tena maana mwenyewe natamani ingekuwa kweli” alisema Linah Sanga.
Katika hatua nyingine msanii huyo kwa sasa anasema ameamua kufanya tu kazi na kuachana na masuala ya mapenzi na kusema kuwa akichanganya kazi na mapenzi mwisho wa siku hata kazi yenyewe anaweza kuharibu.
Linah amedai mpaka sasa ana mipango ya kufanya kazi na Wizkid ingawa anadai kwa sasa alimwambia yupo ‘busy’ kidogo mpaka siku za usoni ndipo wanaweza kukamilisha kazi hiyo.
CHANZO Eatv.tv
0 comments:
Post a Comment