Ulinzi umeimarishwa katika ukumbi ambao matokeo ya uchaguzi mkuu wa marudio visiwani Zanzibar yatatangazwa.
Mbwa wa ulinzi pia wametumika kukagua eneo hilo, ambalo mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar Selim Jecha Selim anatarajiwa kutumia kutangaza matokeo baadaye leo.
Tume hiyo bado haijasema ni saa ngapi matokeo ya kwanza yataanza kutangazwa Ingawa leo jioni kuna dalili zote kuwa matokeo yatatangazwa
Mwenyekiti huyo alitupiwa lawama nyingi na upinzani kwa kufuta matokeo ya uchaguzi wa Oktoba 25.
Licha ya kususia uchaguzi huu wa marejeo na kusema kuwa si halali, bado chama cha wananchi CUF kiliwekwa katika orodha ya washiriki katika zoezi hilo lililofanyika jana.
CUF Kiliuelezea uchaguzi huo kuwa ni batili.
Idadi ya waliojitokeza kushiriki uchaguzi huo wa Jumapili ilikuwa ndogo.
Zanzibar ina jumla ya wapiga kura 503,860 waliojiandikisha kupiga kura, kwa mujibu wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar.
Kulikuwa na wagombea 14 kwenye karatasi za kura za kumchagua rais. Majina yao ndiyo haya:
1 | Khamis Iddi Lila | ACT-W |
2 | Juma Ali Khatib | ADA-TADEA |
3 | Hamad Rashid Mohamed | ADC |
4 | Said Soud Said | AFP |
5 | Ali Khatib Ali | CCK |
6 | Ali Mohamed Shein | CCM |
7 | Mohammed Massoud Rashid | CHAUMMA |
8 | Seif Sharif Hamad | CUF |
9 | Taibu Mussa Juma | DM |
10 | Abdalla Kombo Khamis | DP |
11 | Kassim Bakar Aly | JAHAZI |
12 | Seif Ali Iddi | NRA |
13 | Issa Mohammed Zonga | SAU |
14 | Hafidh Hassan Suleiman | TLP |
0 comments:
Post a Comment