MABINGWA wa Tanzania Bara Yanga Leo wakiwa Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam wakicheza Mechi ya Pili ya Raundi ya Mtoano ya Timu 32 ya CAF CHAMPIONZ LIGI dhidi ya Armee Patriotique Rwandaise FC walitoka Sare 1-1 na kusionga Raundi ijayo kwa vile walishinda Mechi ya Kwanza Bao 2-1.
Katika Mechi ya Kwanza iliyochezwa huko Kigali, Rwanda, Yanga iliitandika APR Bao 2-1 kwa Bao za Juma Abdul na Thaban Kamusoko.
Leo Yanga walianza vibaya kwa kupigwa Bao Dakika ya 4 tu lakini Donald Ngoma akasawazisha Dakika ya 28 na kuwaingiza Raundi ya mwisho ya mtoano ambayo watapambana na Mshindi kati ya Al Ahly ya Egypt na Recreativo de Libolo ya Angola ambazo nazo Leo zinacheza Mechi ya Pili huko Borg El Arab Stadium Mjini Alexandria Nchini Misri baada kutoka 0-0 huko Angola.
CAF CHAMPIONS LEAGUE
Raundi ya Mtoano ya Timu 32 – Mechi za Pili
RATIBA/MATOKEO:
**Saa za Bongo.
**Kwenye Mabano Jumla ya Mabao kwa Mechi mbili
Cnaps Sports – Madagascar 2 Wydad Athletic Club – Morocco 1 [3-6]
Vitalo FC – Burundi 2 Enyimba International FC – Nigeria 1 [3-6]
Young Africans – Tanzania 1 Armee Patriotique Rwandaise FC – Rwanda 1 [3-1]
**Kwenye Mabano Matokeo Mechi ya Kwanza
17:30 AC Leopards de Dolisie – Congo v Mamelodi Sundowns - South Africa
18:30 ES Sahel – Tunisia v Olympique Club De Khouribga – Morocco [1-1]
19:00 Al Ahly – Egypt v Recreativo de Libolo - Angola [0-0]
21:00 El Merreikh - Sudan v Warri Wolves – Nigeria [1-0]
18:00 Al Zamalek – Egypt v Union Sportive de Douala - Cameroon
0 comments:
Post a Comment