Thursday, 10 March 2016

Mbunge wa Ubungo akisimulia alivyokamatwa na Polisi kwa tuhuma za vurugu uchaguzi wa Meya

Leo March 10 2016 Mbunge wa Jimbo la Ubungo (Chadema), Saed Kubeneaamehitajika polisi kwa tuhuma za kuhusika na vurugu  wakati uchaguzi huo ulipoahirishwa February 27 2016. Saed Kubenea ameelezea kuhusiana na wito huo wa polisi kwa ajili ya kujibu tuhuma hizo na amesimulia ilivyokuwa…
Nimefuatwa na askari kama sita wakiniambia kwamba niko chini ya ulinzi ninahitajika makao makuu ya polisi Dar es salam nikahoji kosa langu ni nini? wakasema nikajibu tuhuma juu ya vurugu zilizotokea katika uchaguzi wa Meya wa Dar es salaam‘:-Saed Kubenea
’Mimi nilifika makao makuu polisi kuwasilisha malalamiko juu ya amri iliyotolewa kwamba uchaguzi ule uzuiliwe, niliwathibitishia Polisi kwamba amri ile ilikuwa haramu na ilikuwa imeexipire kwa hiyo ni lazima wachukue hatua za kisheria dhidi ya wahusika‘:-Saed Kubenea

0 comments: