Watu 31 wamefariki baada ya mashambulio kutekelezwa katika uwanja wa ndege wa Zaventem na kituo cha treni cha Maelbeek mjini Brussels.
Waziri wa afya wa Ubelgiji amesema watu 11 walifariki na wengine 81 kujeruhiwa baada ya milipuko miwili kutokea uwanja wa ndege wa Zaventem, nje kidogo ya mji wa Brussels.
Meya wa Brussels amesema watu 20 walifariki Maelbeek.
Kundi linalojiita Islamic State limedai kutekeleza mashambulio hayo
Waziri Mkuu wa Ufaransa Francois Hollande amelaani mashambulio hayo mjini Brussels na kusema ni kama mashambulio yaliyolenga bara lote la Ulaya.
Waziri Mkuu wa Ubelgiji Charles Michel amesema hatua zaidi zimechukuliwa kuimarisha usalama mpakani.
- Kwa Picha: Mashambulio ya Brussels
- Mshukiwa wa Paris alitaka kujilipua
- Mchezaji wa DR Congo anusurika Brussels
Milipuko hiyo imetokea siku nne tu baada ya kukamatwa kwa mshukiwa mkuu wa mashambulio ya Paris ya mwaka jana ambayo yalisababisha vifo vya watu 130.
Abdeslam alikamatwa Ijumaa katika mtaa mmoja wa Brussels.
Uwanja wa ndege wa Zaventem unapatikana kilomita 11 kaskazini mashariki mwa Brussels na ulihudumia abiria zaidi ya 23 milioni mwaka jana.
Watu zaidi ya 30 wamefariki baada ya milipuko mitatu kutokea katika mji wa Brussels nchini Ubelgiji.
- Watu zaidi ya 30 wamefariki baada ya milipuko mitatu kutokea katika mji wa Brussels nchini Ubelgiji.
- Watu 11 walifariki kutokana na milipuko miwili katika uwanja wa ndege wa Zaventem, nje kidogo ya mji wa Brussels.
- Maafisa wa huduma za dharura wakishirikiana na maafisa wa usalama waliwaondoa watu wote uwanja huo wa ndege.
- Mlipuko mwingine ulitokea kituo cha treni cha Maelbeek.
- Watu 20 walifariki katika kituo hicho cha treni, kwa mujibu wa meya wa Brussels.
- Picha zilizosambazwa katika mitandao ya kijamii zimeonesha watu wakiukimbia uwanja wa ndege wa Zaventem baada ya milipuko kutokea.
- Safari za ndege uwanja huo wa kimataifa wa Brussels zimesitishwa.
- Uchukuzi wa treni na mabasi katika mji wa Brussels pia ulisitishwa na raia wakatakiwa kusalia manyumbani.
- Kundi la Islamic State limedai kutekeleza mashambulio hayo ambayo yametokea siku nne tu baada ya kukamatwa kwa mshukiwa mkuu wa mashambulio ya Paris Salah Abdesalam aliyekamatwa Brussels Ijumaa.
- Watu zaidi ya 100 walijeruhiwa kwenye mashambulio hayo.
- Watu wamekuwa wakiandika ujumbe kwenye barabara kuwakumbuka waathiriwa.
- "Pole Brussels" linasema bango hili.
0 comments:
Post a Comment