wilayani mlele
Na Kibada Kibada -Mpanda Katavi
………………………………………………………..
Zaidi ya watoto 2000 wamebainika
kuwa wanaishi katika mazingira hatarishi katika kaya 650 Wilayani Mlele
Mkoa wa Katavi na wako hatarini kukosa huduma za msingi kama Elimu,Afya
,Maji,Ulinzi na Malazi.
Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi
wa Asasi ya Kiraia inayojishughulisha na shughuli za Maendeleo ya
Kijamii katika Wilaya ya Mlele Usevya Development Society (UDESO) Aden
Wanyimba alipokuwa akizungumza na waandishi wa Habari hapo jana kwenye
ukumbi wa Mikutano Ofisi ya Mkoa wa Katavi.
Wanyimba alieleza kuwa Taasisi ya
(UDESO) inayojishughulisha na Shughuli za utetei na ushawishi kwa
watoto wanoishi katika mazingira hatarishi, uhifadhi wa mazingira
,kudhibiti wa maambukizi ya Ukimwi na kukuza Elimu.
Pia Taasisi hiyo kupitia mradi wa
Pamoja Tuwalee imepanga kuwafikia watoto 2119 wanaoishi katika
mazingira hatarishi katika kaya 650 Wilayani Mlele ili kuhakikisha
watoto wanapata huduma za msingi za kijamii.
by John Bukuku on January 3, 2014 in JAMII
0 comments:
Post a Comment