Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) limewapatia beji waamuzi kumi wa Tanzania kwa mwaka 2014.
Waamuzi wa kati waliopata beji hiyo ni Ramadhan Ibada, Oden Mbaga, Israel Mujuni na Waziri Sheha.
Waamuzi
wasaidizi ni Josephat Bulali, Ferdinand Chacha, Hamis Changwalu, John
Kanyenye, Ali Kinduli, Erasmo Jesse na Samuel Mpenzu.
WATATU WAOMBEWA ITC SHELISHELI
Shirikisho
la Mpira wa Miguu la Shelisheli (SFF) limetuma Shirikisho la Mpira wa
Miguu Tanzania (TFF) maombi ya Hati ya Uhamisho ya Kimataifa (ITC) kwa
wachezaji watatu wa Tanzania.
Wachezaji
walioombewa hati hiyo ili wakajiunge na timu ya La Passe FC inayocheza
Ligi Kuu nchini humo ni Salum Kinje aliyekuwa akiichezea timu ya Simba,
Semmy Kessy aliyekuwa Lipuli ya Iringa na Rashid Gumbo aliyekuwa timu ya
Mtibwa Sugar.
TFF inafanyia kazi maombi hayo na mara taratibu zitakapokamilika hati hizo zitatolewa.
Boniface Wambura Mgoyo
Ofisa Habari na Mawasiliano
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
0 comments:
Post a Comment