Saturday, 25 January 2014

VPL: TANZANIA YANGA MBEYA CITY NA AZAM WAENDELEZA USHINDI ANGALIA MATOKEO YA MECHI ZOTE

>>AZAM YAITUNGUA MTIBWA, COASTAL SARE NA OLJORO!!
>>MBEYA CITY KIDEDEA HUKO KAITABA!
>>JUMAPILI: SIMBA v RHINO RANGERS, UWANJA WA TAIFA!
MATOKEO:
Jumamosi, 25 Januari 2014
Ashanti United 1 Yanga 2
Azam FC 1 Mtibwa Sugar 0
Coastal Union 1 JKT Oljoro 1
Kagera Sugar 0 Mbeya City 1

ASHANTI 1 YANGA 2
VPL_2013-2014-FPMabingwa Watetezi wa VPL, Ligi Kuu Vodacom, leo imebidi wajitutumue na kuibwaga Ashantu United Bao 2-1 katika Mechi ya Kwanza ya Ligi Mzunguko wa Pili iliyochezwa Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.
Bao zote za Mechi hii zilifungwa katika Kipindi cha Pili kwa Yanga kutangulia kwa Bao la Kavunbagu katika Dakika ya 51 lakini Ashanti wakasawazisha katika Dakika ya 61 kwa Bao la Mchezaji wa Nigeria, Bright Obinna.
Yanga walifunga Bao lao la ushindi katika Dakika ya 80 kwa mzinga wa David Luhende.
Ushindi huu umeibakisha Yanga kileleni wakiwa na Pointi 31, Pointi 1 mbele ya Azam FC ambao nao leo waliishinda Mtibwa Sugar Bao 1-0.
VIKOSI:
YANGA: Deo Munishi, Juma Abdul, Oscar Joshua, Mbuyu Twite, Kevin Yondan, Frank Domayo, Mrisho Ngassa,Haruna Niyonzima, Didier Kavumbangu, Said Bahanuzi, David Luhende.
Akiba: Ally Mustafa "Barthez", Nadir Haroub "Cannavaro", Hamis Thabit, Nizar Khalfani, Hussein Javu, Saimon Msuva, Jerson Tegete
ASHANTI: Daudi Mwasongwe, Hussein Mkongo, Abdul Mtiro, Shaffi Hassan, Tumba Swedi, Mohammed Fakhi, Abdul Manani, Fakih Hakika, Bright Obinna, Hussein Swedi, Joseph Mahundi.
AZAM FC 1 MTIBWA SUGAR 0
Bao la Mchezaji hatari, Kipre Tchetche, leo limeipa ushindi Azam FC wa Bao 1-0 walipocheza na Mtibwa Sugar huko Azam Complex kwenye Viunga vya Jiji la Dar es Salaam.
Ushindi huu umeifanya Azam FC ijichimbie Nafasi ya Pili ikiwa na Pointi 30, Pointi 1 nyuma ya Vinara Yanga.
   
COASTAL UNION 1 JKT OLJORO 1
Katika Mechi nyingine ya Ligi iliyochezwa hii leo huko Mkwakwani Jijini Tanga, Coastal Union na JKT Oljoro zilitoka Sare ya Bao 1-1.
Goli la Coastal Union lilifungwa na Yaya Kato Lutimba katika Dakika ya 5 na JKT Oljoro kusawazisha Dakika ya 90
LIGI KUU VODACOM
RATIBA:
Jumapili, 26 Januari 2014
JKT Ruvu v Mgambo JKT
Simba v Rhino Rangers
MSIMAMO:
NO
TEAMS
P
W
D
L
GF
GA
GD
PTS
1
Young Africans
14
9
4
1
33
12
21
31
2
Azam FC
14
8
6
0
24
10
14
30
3
Mbeya City
14
8
6
0
21
11
10
30
4
Simba SC
13
6
6
1
26
13
13
24
5
Kagera Sugar
14
5
5
4
15
11
4
20
6
Mtibwa Sugar
14
5
5
4
19
18
1
20
7
Coastal Union
14
3
8
3
11
8
3
17
8
Ruvu Shootings
13
4
5
4
15
15
0
17
9
JKT Ruvu
13
5
0
8
10
16
-6
15
10
Rhino Rangers
13
2
5
6
9
16
-7
11
11
JKT Oljoro
14
2
5
7
10
11
-10
11
12
Ashanti United
14
2
4
8
13
26
-13
10
13
Tanzania Prisons
13
1
6
6
6
16
-10
9
14
Mgambo JKT
13
1
3
9
3
23
-20
6

0 comments: