WILAYA YA MBOZI – MAUAJI.
MNAMO
TAREHE 14.01.2014 MAJIRA YA SAA 07:00HRS HUKO KIJIJI CHA HANSETWA, KATA
YA IHANDA, TARAFA YA VWAWA, WILAYA YA MBOZI, MKOA WA MBEYA, IRENE D/O
MWAMLIMA, MIAKA 69, MNYIHA, MKULIMA NA MKAZI WA HANSETWA ALIKUTWA
AMEUAWA KWA KUKATWA NA KITU KINACHODHANIWA KUWA NI PANGA SEHEMU ZA
KISOGONI, USONI NA KUVUNJWA TAYA NA MTU/WATU WASIOFAHAMNIKA. MAREHEMU
ALIKUWA AKIISHI PEKEE YAKE, CHANZO CHA MAUAJI HAYO NI IMANI ZA
KISHIRIKINA. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI
MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA
KUAMINI IMANI POTOFU ZA KISHIRIKINA KWANI ZINA MADHARA MAKUBWA KATIKA
JAMII. AIDHA ANATOA WITO KWA MTU YEYOTE MWENYE TAARIFA ZA MAHALI ALIPO
MTU/WATU WALIOHUSIKA NA TUKIO HILI AZITOE ILI KUFANIKISHA KUKAMATWA NA
SHERIA ICHUKUE MKONDO WAKE.
WILAYA YA MBEYA VIJIJINI – KUPATIKANA NA BHANGI.
MNAMO
TAREHE 14.01.2014 MAJIRA YA SAA 10:30HRS HUKO MAENEO YA MBALIZI KATA YA
UTENGULE TARAFA YA USONGWE MBEYA VIJIJINI ASKARI POLISI WAKIWA DORIA
WALIMKAMATA MWILE S/O MUWANGO, MIAKA 30, MMALILA, MKAZI WA NDOLA AKIWA
WA BHANGI KETE 58 SAWA NA UZITO WA GRAMU 290 NDANI YA MFUKO WA MWEUSI
AKIWA ANAUZA, MTUHUMIWA NI MUUZAJI NA MTUMIAJI WA BHANGI HIYO. KAMANDA
WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z.
MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA KUTUMIA DAWA ZA KULEVYA KWANI NI
KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI.
WILAYA YA MBEYA MJINI – KUPATIKANA NA BHANGI.
MNAMO
TAREHE 14.01.2014 MAJIRA YA SAA 12:00HRS HUKO KABWE KATA YA IYELA
TARAFA YA IYUNGA JIJI NA MKOA WA MBEYA. ASKARI POLISI WAKIWA DORIA
WALIMKAMATA EDWIN S/O ALINANI, MIAKA 24, MKINGA NA MKAZI WA MAKUNGURU
AKIWA NA BHNAGI KETE 13 SAWA NA UZITO WA GRAMU 65 NDANI YA MFUKO WAKE WA
SURUALI. MTUHUMIWA NI MUUZAJI NA MTUMIAJI WA BHANGI HIYO. KAMANDA WA
POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z.
MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA KUTUMIA DAWA ZA KULEVYA KWANI NI
KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI.
WILAYA YA MBEYA VIJIJINI – KUPATIKANA NA POMBE HARAMU YA MOSHI
[GONGO].
MNAMO
TAREHE 14.01.2014 MAJIRA YA SAA 13:45HRS HUKO KITONGOJI CHA MSHIKAMANO,
KATA YA NSALAGA, TARAFA YA USONGWE, MBEYA VIJIJINI ASKARI POLISI
WAKIWA DORIA/MSAKO WALIMKAMATA PIUS S/O LAPACHI, MIAKA 20, MBUNGU NA
MKAZI WA NDOLA AKIWA NA POMBE YA MOSHI UJAZO WA LITA 1 ½. MTUHUMIWA
NI MTUMIAJI WA POMBE HIYO. TARATIBU ZA KISHERIA ZINAFANYWA ILI AFIKISHWE
MAHAKAMANI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI
MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA
KUTUMIA POMBE HARAMU YA MOSHI KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI
KWA AFYA YA MTUMIAJI.
Imesainiwa na,
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
0 comments:
Post a Comment