>>BAO LA STARS LILIFUNGWA NA MCHA KHAMIS!!
>>TAIFA STARS KUREJEA LEO JIONI KUTOKA NAMIBIA!!
Nae Mchezaji alietoka Benchi, Mcha
Khamis, aliifungia Taifa Stars Bao Dakika 3 kabla Mpira kumalizika
kufuatia Kona lakini Nekundi alifunga kwa Kichwa baada ya Frikiki
iliyopigwa na Petrus Shitembi Dakika 5 ndani ya Dakika za Majeruhi.
Mechi hii ilishuhudiwa na Watu wasiozidi
2000 kwenye Uwanja wa Sam Nujoma na Watazamaji hao hawakuwa na furaha
yeyote baada ya Timu yao kushindwa kutengeneza nafasi yeyote ya kufunga.
[RIPOTI NA PICHA TOKA THE MAMIBIAN]
Release No. 038
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Machi 6, 2014
TAIFA STARS KUREJEA MCHANA KUTOKA NAMIBIA
Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars)
inatarajia kurejea Leo Jioni Saa 12 Dakika 45 kutoka Windhoek, Namibia
kwenye mechi ya kirafiki ya kalenda ya FIFA.
Taifa Stars ambayo katika mechi hiyo
dhidi ya Namibia (Brave Warriors) ilitoka sare ya bao 1-1 itatua Uwanja
wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) kwa ndege ya South Africa
Airways.
Timu inayodhaminiwa na Kilimanjaro
Premium Lager baada ya kuwasili itakwenda hoteli ya Accomondia kwa ajili
ya chakula cha mchana na baadaye kuvunja rasmi kambi yake.
Boniface Wambura Mgoyo
Media and Communications Officer
Tanzania Football Federation (TFF)
0 comments:
Post a Comment