Thursday, 16 January 2014

SIMBA NA MTIBWA SUKARI KESHO KIINGILIO SH.5000


MABINGWA wa michuano ya mtani Jembe, timu ya Simba,images
kesho  inashuka katika Uwanja wa Taifa kuvaana na timu ya

Mtibwa Sugar, huku kiingilio cha chini kikiwa sh.5000.

Mchezo huo utakaoanza saa 10 jioni, ukiwa wa kirafiki,

kwa ajili ya kuziweka timu hizo sawa kabla ya kuanza kwa

Ligi Kuu tanzania Bara, inayoanza kutimua vumbi wiki

ijayo.

Simba inaingia dimbani ikiwa inatoka kwenye mashindano

ya Mapinduzi, ambapo Simba ilichukua ushindi wa pili.

Katika mchezo huo Simba iliyopo chini ya kocha Zdravko

Logarusic akisaidiana na Suleiman Matola, imepanga

kutumia wachezaji wake, wote ili kiwe kipimo tosha kabla

ya Ligi Kuu.

Timu hiyo inayoshika nafasi ya nne katika msimamo wa

Ligi, imejipanga kuhakikisha inavuka mpaka nafasi ya

kwanza huku kocha wao Logarusic, akisema ana uhakika

kikosi chake kitaibuka na ushindi.

Logarusic, alisema kuwa mchezo huo ni moja ya mtihani

wake wa kutambua kikosi chake, kabla ya kuanza kwa ligi

kuu.

Alisema ameambiwa kuwa Mtibwa Sugar, ni moja ya timu

nzuri hivyo anajua kwake ni kipimo kizuri.

“Nina amini mchezo wetu na Mtibwa Sugar, utakuwa mzuri

, kutokana na ubora wa timu hiyo, ninajua itasaidia timu

yangu kupata mazoezi mazuri”alisema Logarusic.

Nae kocha wa Mtibwa Sugar, Mecky Mexime, alisema ana

amini mchezo huo utakuwa mzuri kwake kutokana na

wapinzani wao kutoka katika mashindano.

Mexime alisema kuwa amepata nafasi ya kucheza na timu

kubwa, ambayo itampa mazoezi mazuri.

“Nina amini mchezo huo utakuwa mzuri kwangu kwa kuwa

nacheza na timu kubwa ambayo imetoka kwenye

mashindano”alisema Mexime.

Katika mchezo huo viingilio vitakuwa shilingi 20,000 VIP A,

shilingi 10,000 katika VIP B, wakati VIP C itakuwa shilingi

7,000 na sehemu ya viti vya orange na bluu itakuwa

shilingi 5000.

Related Posts:

0 comments: