Monday, 6 January 2014

SHABIKI ACHOMWA KISU ANFIELD NA MOYES AHAKIKISHIWA FEDHA KUNUNUA WAPYA!

SHABIKI ACHOMWA KISU ANFIELD!
ANFIELD_1Shabiki wa Oldham alichomwa Kisu hapo Jana baada ya pambano la Liverpool na Oldham la Raundi ya Tatu ya FA CUP lililochezwa Anfield na Liverpool kushinda Bao 2-0.
Polisi wa Kitongoji cha Merseyside walisema Mtu mmoja mwenye Umri wa Miaka 35 alisimamisha Ambulensi iliyokuwa ikipita jirani na maeneo ya Uwanja wa Anfield mara baada ya Mechi hiyo.
Hata hivyo Polisi wamesema Shabiki huyo aliechomwa Kisu ambae yuko salama amekataa kusema chochote kwa Polisi.
Polisi imewataka Mashahidi walioshuhudia tukio hilo wajitokeze kutoa Taarifa.
MOYES AHAKIKISHIWA FEDHA KUNUNUA WAPYA!
Meneja wa Manchester United David Moyes amehakikishiwa kuwa zipo Fedha za kununuaMOYES-NGUMI_JUUWachezaji wakati huu wa Dirisha la Uhamisho la Januari na pia mwishoni mwa Msimu.
Inaaminika Klabu inalenga kumnunua Fulbeki wa Kushoto na Kiungo mmoja lakini hawatahaha kununua Mchezaji ili mradi kununua tu bali watalenga Wachezaji Bora wanaokidhi viwango vyao.
Mara baada ya kufungwa hapo Jana Bao 2-1 na Swansea City na kutupwa nje ya FA CUP, David Moyes alikiri Timu inahitaji nguvu mpya ya Wachezaji wapya lakini alisema: “Tunataka kuleta Wachezaji lakini Wachezaji hao wanapatikana? Upo umuhimu lakini Wachezaji tunaowataka hawapatikani Mwezi Januari.”
Man United bado hawajafungua Kipengele cha kuwaongezea Mikataba ya Mwaka mmoja mmoja ya Rio Ferdinand na Patrice Evra, ambao Mikataba yao inamalizika mwishoni mwa Msimu na pia hawajazungumza na Nemanja Vidic na Fabio ambao Mwezi huu, Kisheria, wako huru kuongea na Klabu nyingine kama wakitaka kuhama.
Lakini duru za ndani ya Man United zimedai mazungumzo na Wachezaji hao wote, pamoja na Wayne Rooney, yatafanyika na hakuna sababu ya kuwa na mchecheto.
Vile vile imefamika zipo Klabu 6 zinamtaka Wilfried Zaha kwa Mkopo Mwezi huu Januari na ingawa Moyes amekiri kuwa Zaha anahitaji kucheza Mechi zaidi ambazo atazipata akienda kwingine kwa Mkopo bado hawajaamua hilo kwa vile Winga Nani ni majeruhi.

Related Posts:

0 comments: