BEKI wa zamani wa Brazil na Real Madrid, Roberto
Carlos, amekaa dakika chache na wachezaji wa Yanga mjini Antalya,
Uturuki na kuwapa somo la maana.
Carlos yuko mjini hapa na timu yake ya Sivasspor
FC inayoshiriki Ligi Kuu Uturuki. Timu ya Carlos inafanya mazoezi kwenye
uwanja mmoja na Yanga na pia inaishi hoteli ya Sueno ilipo Yanga.
Gwiji huyo anayeheshimika kwa mafanikio yake
aliyoyapata akitumia mguu wa kushoto, alishituka baada ya kusikia Yanga
inatoka Tanzania ambako aliwahi kufundisha Kocha Mbrazili, Marcio
Maximo, ambaye yeye anamheshimu sana.
Carlos alipiga picha na wachezaji wa Yanga halafu
baadaye yeye na timu yake wakaangalia mazoezi ya wana Jangwani hao kwa
dakika kumi kisha akakaa nao na kuzungumza kidogo na kuwachangamkia.
“Nimefurahi sana kusikia kwamba mmetoka Tanzania
alikokuwa anafundisha Maximo (kocha wa zamani wa Taifa Stars),
ninamheshimu sana yule kocha,” aliwaambia wachezaji wa Yanga.
“Ni katika watu muhimu sana kwangu, wachezaji
nimewafurahia mnavyocheza. Mnachotakiwa kufanya ni kuongeza juhudi
mkitambua kwamba kila mmoja ana nafasi yake ya kuonekana.”
Kocha anayeiongoza Yanga kwa sasa, Boniface
Mkwasa, alisema mazoezi ambayo kikosi chake imeyaanza juzi Ijumaa,
yatasaidia kuiweka timu katika hali nzuri na kuwa tayari kwa mashindano.na jana Jumamosi Yanga ilitacheza mechi ya kujipima nguvu na Ankara Sekerspor
ya Ligi Daraja la Pili Uturuki na yanga kuibuka mshindi wa bao 3-0 .By MWANDISHI chanzoWETU, ANTALYA mwanasport gazeti
0 comments:
Post a Comment