![]() |
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Naibu Rais wa Kenya Mhe William Ruto walipowasili kwa pamoja katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta jijini Nairobi leo |
![]() |
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Naibu Rais wa Kenya Mhe. William Ruto
waliwasili kwa pamoja katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo
Kenyatta jijini Nairobi leo Ijumaa Januari 24, 2014.
Viongozi hawa walikutana jijini Amsterdam, Uholanzi, na kupanda ndege moja kuelekea nyumbani.
Rais Kikwete ambaye alitua Nairobi kwa muda akitokea Davos, Uswisi, alikokuwa kwenye ziara ya kikazi ambayo ameikatisha ili kujiunga na wananchi wa jimbo la Chalinze katika msiba wa Mbunge wa jimbo hilo Marehemu Said Bwanamdogo. Mazishi yamepangwa kufanyika leo nyumbani kwa marehemu Miono, Bagamoyo.

0 comments:
Post a Comment