.
Mmoja kati ya watoto waliofanyiwa ukatili wa kinyama (picha na maktaba yetu)
..........................................
HABARI HII IMENUKURI WA KUTOKA KWA FRANCIS GODWIN NA DIANA BISANGAO WA MATUKIO DAIMA.COM, IRINGA
JESHI la polisi mkoani Iringa linamshikilia mwanamke mmoja
mkazi wa Iramba kata ya Itundula wilaya ya Mufindi kwa kumchinja shingo mtoto wake na kumtupa chooni
Akizungumza na mtandao huu w kamanda wa polisi
mkoani Iringa Ramadhan Mungi alithibitisha kutokea kwa tukio hilo.
Kamanda Mungi alimtaja mwanamke huyo kwa jina la
Restuta Mdemu ambae umri wake haujafahamika alijifungua mtoto mwenye jinsia ya kiume
muda kabla ya kumuua kinyama kwa kumchinja shingo yake na kumtupa chooni .
Aidha alisema kuwa mwanamke huyo alimuua
mtoto wake kwa kumchinja shingoni na kitu chenye ncha kali kwa sababu anazozijua yeye mwenyewe .
Chanzo cha tukio hilo
la mauaji ya kinyama kwa mtoto huyo bado hakijafahamika.
0 comments:
Post a Comment