MTOTO
ZAINA HEMED AMBAYE NI WADARASA LA SABA KATIK SHULE YA MSINGI BUGURUNI
VIZIWI AKIZUNGUMZA KWA NIABA YA WATOTO WOTE KATKA MKUTANO HUO ALIKUWA NA
MKALIMAN AMBAYE KWENYE PICHA HAONEKANI
......................................................................................................................
Mwandishi Kenneth John wa ,Dar
......................................................................................................................
Mwandishi Kenneth John wa ,Dar
Serikali
ya Tanzania kwa
kushirikiana na mfuko
wa maendeleo ya
watoto wa umoja
wa mataifa (UNICEF), ujumbe wa
umoja wa ulaya
(EU) Tanzania ,Shirika la
save chidren pamoja
na shirika la
Plan International (PLAN) leo
wamezindua mpango wa
pamoja wa kukomesha
ukatili dhidi ya
watoto Tanzania.
Akizungumza
katika uzinduzi huo
waziri wa afya
na ustawi wa
jamii Dkt Seif
Rashid alisema kuwa
kila hamashauri zinawajibu
wa kusajili watoto
wote ambao wanaishi
katika mazingira hatarishi , pamoja na
kutoa taarifa za
matokeo yote ambayo
yanaenda sambamba na
kusababisha athari kwa
watoto.
Pia aliongeza kuwa
kunahitajika kuwa na
maafisa jamii ambao
wanauwezo wa kuhakikisha
wanampa ushirikiano wa
kutosha mtoto pamoja
na kuzungumza na
mtoto kwa uwazi
zaidi.
Mradi
huo unalengo la
kusaidia uanzishwaji wa
mifumo ya kumlinda
mtoto ili kuweza
kudhibiti na kukabiliana
na kila aina
ya ukatili dhidi
ya watoto , hasa watoto
wa kike na
hatua hiyo itasaidia
utekelezaji wa mipango
iliyopo ya kupambana
na ajira kwa
watoto pamoja na
kuanzisha shule salama
Zanzibar.
Aidha mradi huo
pia unalengo la
kusaidia watoto na
familia zao,kuimarisha ulinzi
katika mazingira ya
jamii na shule
salama, pia mradi umelenga
kufikia malengo ya
muda mrefu,kuwa na
mfumo wenye jukumu
la mstari wa
mbele pamoja na
kuwa na mfumo
endelevu kwa ajili
ya kutambua, kuzuia ,
kukabiliana na kusaidia
watoto kwa kuujumuisha
katika mfumo wa
mamlaka za serikali
za mitaa na
taratibu za jamii
kwa kutumia ,matokeo
yatakayopatikana kuhamasisha mgao
wa mara kwa
mara wa bajeti
kwaajili ya ulinzi
wa mtoto katika
ngazi ya wilaya
na katika ngazi
ya kitaifa.
Na kwa upande
wa mwakilishi wa
UNICEF nchini Dkt
Jama Gulaid alisema
kuwa ushirikiano huo
ni hatua muhimu
ya kuimarisha mifumo
ya ulinzi wa
watoto ilikukabiliana na
ukatili dhidi ya
watoto nchini,pamoja na
kutoa fursa ya
kuimarisha muungano kwaajili
ya maendeleo ya
watoto katika ya
Umoja wa Ulaya,
Pamoja
na hayo yote
kwa mujibu wa
ripoti ya utafiti
wa ukatili dhidi
ya watoto Tanzania
uliotolewa na serikali
ya na UNICEF
mwaka 2011 ulidhihirisha kwamba
msichana mmoja kati
ya watatu na
mvulana mmoja kati
ya saba nchini
Tanzania hukubwa na
manyanyaso ya kijinsia
kabla ya kufikisha
umri wa miaka
kumi nane,Pia tafiti
ilibaini kuwa viwango
vya unyanyasaji wa
kimwili viko juu
sana kwani karibu
wasichana na wavulana
watatu kati ya
wanne wamepigwa ngumi, kuchapwa au
kupigwa mateke wakati
wa utoto wao, huku
robo ya watoto
wote wamefanyiwa ukatili
wa kihisia,na ripoti
hiyo ilionyesha kuwa
watoto wengi hawashtaki
matukio hayo,wachache hutafuta
huduma stahiki na wachache zaidi
hupatiwa huduma ya
matibabu au msaada.
0 comments:
Post a Comment