Sunday, 2 February 2014

SERIE A: JUVE POINTI 9 MBELE, YAICHAPA INTER MILAN 3-1!

JUVE_UBINGWAMABINGWA na Vinara wa Serie A huko Italy, Juventus, Jana Usiku wamepaa na kuwa Pointi 9 mbele baada ya kuwapa Inter Milan kipigo cha Bao 3-0 kwenye Mechi ya Ligi iliyochezwa Juventus Stadium.
Pengo hilo la Juve limekuwa kubwa kufuatia ushindi huo na hasa baada ya Timu ya Pili, AS Roma, kushindwa kumaliza Mechi yao hiyo Jana na Parma baada Mechi kuvunjwa katika Dakika ya 8 kufuatia Uwanja kujaa maji baada Mvua kubwa na pia Timu ya Tatu, Napoli kubamizwa Bao 3-0 na Atalanta mapema Jana.
Bao za Juve zilifungwa na Stephan Lichtsteiner, Giorgio Chiellini na Arturo Vidal huku Inter Milan wakipata Bao lao kupitia Rolando.
 
MATOKEO:
Jumapili Februari 2
Atalanta 3 Napoli 0
Chievo Verona 0 Lazio 2
AS Roma v Parma [Mechi imevunjwa sababu ya Mvua]
Catania 3 Livorno 3
Sassuolo 1 Hellas Verona 2
Juventus 3 Inter Milan 1
MSIMAMO-Timu za Juu:
NA TIMU P W D L F A GD PTS
1 Juventus FC 22 19 2 1 54 16 38 59
2 AS Roma 21 15 5 1 45 11 34 50
3 SSC Napoli 22 13 5 4 44 26 18 44
4 ACF Fiorentina 22 12 5 5 40 24 16 41
5 Hellas Verona 22 11 2 9 37 35 2 35
6 Inter Milan 22 8 9 5 39 27 12 33
7 Torino FC 22 8 9 5 35 28 7 33
8 Parma FC 21 8 8 5 32 27 5 32
9 SS Lazio 22 8 7 7 29 29 0 31
10 AC Milan 22 7 8 7 35 32 3 29
11 Genoa CFC 21 7 6 8 23 27 -4 27

0 comments: