RPC Mungi
AMA kweli wivu ni kidonda mwanaume
mmoja mkazi wa kijiji kijiji cha Imalutwa kata ya Lugalo tarafa
ya Mazome wilaya ya Kilolo mkoani Iringa kuua mkewe mjamzito kwa
kumcharaza fimbo hadi kifo kwa wivu wa kimapenzi .
Imedaiwa kuwa mwanaume huyo Vicent
Kasenegala (40) aliingiwa na wivu wa kimapenzi na kuamua kuanza
kumcharaza fimbo za tumbo mkewe kufuatia tabia ya mwanamke huyo
kuhisiwa kuwa na mahusiano ya kimapenzi na rafiki zake wa karibu.
Hivyo kutokana na hisia hizo Kasenegala
aliamua kuchukua uamuzi wa kutoa adhabu kali kwa mkewe kwa kuanza
kumcharaza fimbo katika maeneo mbali mbali ya mwili wake zikiwemo
fimbo za tumbo .
Kamanda wa polisi wa mkoa wa
Iringa Ramadhan Mungi aliuthibitishia mtandao huu wa
www.francisgodwin.blogspot.com kutokea tukio hilo leo wakati
akizungumza na mtandao huu wa www.matukiodaima.com ofisini kwake na
kuwa tukio hilo lilitokea January 7 majira ya saa 10 jioni mwaka huu
katika kitongoji cha Malawi kijiji cha Imalutwa .
Hata hivyo alisema kuwa mtuhumiwa
huyo Bw Kasenegala anatuhumiwa kumuua mkewe Laurencia Chusi (33) ambae
alikuwa akijishughulisha na shughuli za kilimo na baada ya tukio
hilo mtuhumiwa huyo akitoweka kusiko julikana na jeshi la polisi bado
linaendelea kumsaka kwa tuhuma za mauwaji .
|
0 comments:
Post a Comment