Sunday, 5 October 2014

UHABA WA NYUMBA ZA WAALIMU WA PUNGUZA UFANISI WAKUFUNDISHA KWA WALIMU


Uhaba wa nyumba za walimu ni sababu moja wapo ambayo inapunguza  ufanisi wa utendaji kazi kwa walimu hivyo hupelekea ufaulu mdogo wa wanafunzi katika shule nyingi za msingi na sekondari Manispaa ya Iringa Mkoani Iringa.
Mwenyekiti wa chama cha walimu (CWT) manispaa ya Iringa Bibi Zawadi Mgongolwa amesema walimu wengi wanaishi maisha ya kupanga nyumba mitaani kutokana na ukosefu wa nyumba katika shule nyingi hivyo kuongeza gharama ya maisha.
Bibi Mgongolwa amesema walimu wengi hushindwa kumudu gharama za kupanga nyumba pindi wanapopangiwa maeneo husika ambapo baadhi yao hujiingiza kwenye vitendo viovu kutokana na umaskini.
Aidha ameziomba  halmashauri zote za Mkoa wa Iringa kuwapatia walimu viwanja ambavyo watalipa kwa awamu kutokana na gharama kubwa ya viwanja hivyo  ili wajenge nyumba na kupunguza ukali wa maisha.
Hata hivyo, umoja wa walimu wametoa wito kwa halmashauri ya manispaa ya Iringa kujenga nyumba kwa kushirikiana na shirika la nyumba Tanzania(NHC) ili walimu waishi kwa bei nafuu itakayosaidia kupunguza ukali wa maisha.

0 comments: