Sunday, 5 October 2014

BPL :CHELSEA BADO YAINDELEA KUONGOZA LIGI ,YAITWANGA ARSENAL 2-0

 PrintPDF
RATIBA/MATOKEO:
Jumapili Oktoba 5
Man United 2 Everton 1
Chelsea 2 Arsenal 0
Tottenham 1 Southampton 0
1815 West Ham v QPR

CHELSEA 2 ARSENAL 0
Chelsea striker Diego Costa
Chelsea wameendelea kujichimbia kileleni mwa Ligi Kuu England walipoichapa Arsenal Bao 2-0 huko Stamford Bridge hii Leo.Mechi hii ilichelewa kuanza kwa Dakika 15 kwa sababu za kiusalama baada ya baadhi ya Mashabiki kurusha Fataki kabla Mechi haijaanza.
Na ilipoanza ikatosha rabsha baada ya Mameneja wa Timu hizo, Jose Mourinho na Arsene Wenger, kukwaruzana wakati Wenger alipochukizwa baada ya Mchezaji wake Alexis Sanchez kuchezewa Rafu na Gary Cahill ambae alipewa Kadi ya Njano na Refa Martin Atkinson.
Chelsea walilazimika kumbadili Kipa wao Courtois katika Dakika ya 24 na kumwingiza Petr Cech baada ya Kipa huyo kugongana na Alexis Sanchez muda mfupi kabla.
Chelsea walifunga Bao lao la kwanza katika Dakika ya 27 kwa Penati ya Eden Hazard iliyotokana na Laurent Koscienly kumchezea Rafu Hazard na kupewa Kadi ya Njano.
Dakika ya 77, bonge la Pasi ndefu ya Fabregas mbele ilishushwa kifuani na Diego Costa na kukabiliana na Kipa Szczesny na kumvisha kanzu kuandika Bao la Pili kwa Chelsea.
VIKOSI:
CHELSEA: Courtois; Ivanovic, Cahill, Terry, Azpilicueta; Matic, Fabregas; Schurrle, Oscar, Hazard; Diego Costa
Akiba: Cech, Zouma, Filipe Luis, Mikel, Willian, Salah, Remy.
ARSENAL: Szczesny; Chambers, Mertesacker, Koscielny, Gibbs; Wilshere, Flamini; Cazorla, Ozil, Sanchez; Welbeck
Akiba: Martinez, Monreal, Coquelin, Rosicky, Oxlade-Chamberlain, Campbell, Podolski
REFA: Martin Atkinson
 Chelsea striker Diego Costa
TOTTENHAM 1 SOUTHAMPTON 0
Wakicheza kwao White Hart Lane, Tottenham wameifunga Southampton Bao 1-0.
Bao la Tottenham lilifungwa na Christian Eriksen katika Dakika ya 40.
VIKOSI:
TOTTENHAM: Lloris, Naughton, Kaboul, Vertonghen, Rose, Capoue, Mason, Lamela, Eriksen, Chadli, Adebayor
Akiba: Soldado, Vorm, Dier, Townsend, Kane, Dembélé, Fazio
SOUTHAMPTON: Forster, Clyne, Fonte, Alderweireld, Bertrand, Davis, Wanyama, Schneiderlin, Tadic, Pellè, Mané
Akiba: Davis, Gardos, Long, Cork, Mayuka, Reed, Targett
REFA: Mike Jones
MSIMAMO
NA
TIMU
P
GD
PTS
1
Chelsea
7
14
19
2
Man City
7
7
14
3
Southampton
7
6
13
4
Man United
7
3
11
5
Swansea
7
2
11
6
Tottenham
7
2
11
7
Arsenal
7
2
10
8
Liverpool
7
0
10
9
Aston Villa
7
-5
10
10
Hull
7
0
9
11
Leicester
7
-1
9
12
Sunderland
7
1
8
13
West Brom
7
-1
8
14
Crystal Palace
7
-2
8
15
Stoke
7
-2
8
16
West Ham
6
0
7
17
Everton
7
-3
6
18
Newcastle
7
-7
4
19
Burnley
7
-7
4
20
QPR
6
-9
4
RATIBA-Mechi zijazo:
 Saa za Bongo
Jumamosi Oktoba 18
1445 Man City V Tottenham
1700 Arsenal V Hull
1700 Burnley V West Ham
1700 Crystal Palace V Chelsea
1700 Everton V Aston Villa
1700 Newcastle V Leicester
1700 Southampton V Sunderland
Jumapili Oktoba 19
1530 QPR V Liverpool
1800 Stoke V Swansea
Jumatatu Oktoba 20
2200 West Brom v Man United Arsene Wenger and Jose Mourinho

0 comments: