Mtoto wa miaka saba afariki mkoani Iringa kwenye ajali ya moto akiwa amelala ndani ya nyumba yao.
Kamanda wa jeshi la polisi mkoani Iringa ACP.Ramadhani Mungi amesema tukio hilo limetokea katika kijiji cha Nzihi wilaya ya Iringa vijijini Mkoani Iringa.
Kamanda Mungi ameongeza kuwa nyumba hiyo ni mali ya Sakwi Mbasha umri miaka 55 mfugaji wa jamii ya Kimasai mkazi wa kijiji cha Nzihi ambapo jumla ya thamani ya mali zilizoteketea kwenye nyumba hivyo bado havijajulikana.
Aidha aesema jeshi la polisi MKoani Iringa linaendelea na uchunguzi wa kubaini chanzo cha kutokea kwa moto uliopelekea maafa ya kifo cha mtoto huyo.

Hata hivyo, Kamanda wa polisi mkoani Iringa amewaasa wakazi wa mkoa wa Iringa kuwa makini na malezi ya watoto wao pia jamii ya wafugaji wa kimasai wawe makini na makazi yao kutokana ufugaji wao wa kuhama hama hali inayopelekea kuwa na nyumba zinazojengwa kwa nyasi.
0 comments:
Post a Comment