Sunday, 5 October 2014

MASHABIKI WA TIMU YA COAST WASWEKWA LUPANGO KISA KUVAA JEZI YA MDHAMINI WA ZAMANI

 
Mashabiki wa timu ya Coastal Union wamejikuta wakiswekwa lupango mjini Tanga leo, kisa wameshangilia wakiwa wamevaa jezi za mdhamini wa zamani.



Taarifa zinaeleza mashabiki hao walikamatwa baada ya uongozi wa sasa wa Coastal Union kuripoti kwa jeshi la Polisi kwamba walikuwa wakiuza jezi za mdhamini wa zamani Bin Slum Tyres kupitia nembo ya Sound.

Lakini polisi walipofika eneo la tukio, mashabiki hao wa Coastal Union waliewaeleza hizo ni jezi zao za msimu uliopita, lakini mwisho wanne kati yao wakakamtwa na kutupwa lupango.

"Kweli kuna wenzetu walikamtwa, lakini mimi sielewi hasa chanzo, kuna mmoja wetu anaweza kulizungumzia hilo suala.
"Tumeshangazwa sana na uongozi kutufungulia kesi polisi na zaidi walisema kama wanataka wenzetu waachiwe, basi tusiingie na jezi za Sound.
"Hivi ni haki kumchagulia shabiki jezi ya kuvaa, kwani mdhamini mpya ameingia mkataba na klabu au mashabiki.

"Lakini hawaoni England mashabiki wa klabu wanavaa hadi jezi za mdhamini wa miaka kumi iliyopita? Ila mimi siwezi kulizungumzia hili zaidi ntakutafutia mwenzetu maana ndiye alifika hadi polisi kuwatoa wenzetu," kilieleza chanzo.
Inaelezwa mashabiki hao walipuuzia walichoelezwa na uongozi na polisi, wakavaa jezi zao na kuingia kuishangilia kwa nguvu Coastal Union hadi ilipoibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Ndanda FC kwa mabao 2-1.
Kumekuwa na mzozo kati ya mashabiki na uongozi, baadhi yao walinyimwa uanachama hali iliyowashangaza watu wengi kwa kuwa klabu zinataka wanachama wengi ili kuingiza kipato na kuongeza changamoto kwa ajili ya maendeleo.
SALEHJEMBE, inaendelea kumsaka mmoja wa hao waliofika kuwatoa wenzao kituo kwa dhamana, halafu itawadodonshea kilichoendelea zaidi kwenye sakata hilo.

0 comments: