Saturday, 4 January 2014

MAZUNGUMZO YA SUDANI KUSINI YAKWAMA (MAMBO YAWA MAGUMU)

 

Matumaini ya kupatikana kwa amani Sudan Kusini yameingia mashakani baada ya mazungumzo ya uso kwa uso ya pande zinazopingana yaliyokuwa yakitarajiwa kufanyika nchini Ethiopia kuchelewa.
Waziri wa Mambo ya nje wa Ethiopia Tedros Adhanom amesema mazungumzo hayo yaliyokuwa yafanyike siku ya jumamosi hayatafanyika kama ilivyokuwa imetarajiwa.
Amesema mikutano inaendelea mjini Adis Ababa ili kuandaa agenda za mazungumzo hayo ya uso kwa uso ya pande zinazopingana.
Mwandishi wa BBC aliyepo Juba anasema mapigano makali yanaendelea. Ambapo pia majeshi yanayomuunga mkono rais Salva Kiir nayo yanajiandaa kwa mashambulizi katika eneo la Bentiu na Bor miji ambayo kwa sasa inashikiliwa na wafuasi wa Riek Machar aliyekuwa makamu wa rais wa zamani.
Amesema pande zote zinajaribu kuimarisha udhibiti wa kijeshi kabla ya kuanza kwa mazungumzo.

0 comments: