Saturday, 4 January 2014

KUNA AMBAO HAWAKUNIIELEWA NILIPOULIZA;VIDOLE VIWILI AU CHADEMA MBILI

Photo: Kuna Ambao Hawakunielewa Nilipouliza; Vidole Viwili Au Chadema Mbili?

Ndugu zangu,

Majuma mawili yaliyopita, baada ya kuiona picha hiyo Zitto Kabwe akiwa Kigoma niliuliza; Ni vidole viwili au Chadema mbili?

Kwangu niliziona ishara ya chama kinachogawanyika. Na leo picha za wafuasi wa Chadema Mahakamani zinathibitisha juu ya nilichokitafakari majuma mawili yaliyopita.

Tafsiri yangu?

Haiyumkini watu wa Chama kimoja mkagawanyika kwa mabango yenye kusomeka; " Zitto Kwanza Chama Baadae" na mengine " Chadema Kwanza Zitto Baadae".  Hapo kuna tatizo, na anayefikiri ni hali ya kawaida nahofia naye ana matatizo katika kufikiri kwake. 

Ndani ya Chademakwa sasa  kuna mgogoro wa kiungozi na ndio maana ya kufikia hata kufikishana mahakamani. Kuna nakisi ya imani pia. Kwamba viongozi nao hawaaminiani. 

Pande zenye kukinzana ni busara zikatambua hilo. Mwisho wa siku ni vema  wote wakatanguliza busara na hekima. Kwa kutambua kuwa, katika yote wayafanyayo, lililo la kwanza si Zitto wala Chadema, bali ni Tanzania. Ndio, Tanzania Kwanza. 

Na nchi yetu hii inahitaji siasa za upinzani zilizo madhubuti.

Maggid Mjengwa.
Iringa.

Maggid Mjengwa.Iringa.

0 comments: