Saturday, 25 January 2014

MATA ATUA NA HELIKOPTA KITUO CHA MAZOEZI CHA MAN UNITED!

>>KUPIMWA AFYA NA KUSAINI MKATABA!
MATA-ATU_NA_HELIKOPTAKIUNGO wa Chelsea Juan Mata amewasili Jijini Manchester ili kupimwa Afya na kukamilisha taratibu za kuhamia Manchester United kama ilivyothibitishwa na Klabu hiyo.
Man United imeposti picha kwenye Mtandao wa Twitter feed ikimwonyesha Mata akipokelewa na Bosi David Moyes mara tu baada ya kutua kwenye Kituo cha Mazoezi cha Carrington.
SOMA HABARI ZA AWALI:

JUAN MATA: MAN UNITED YATHIBITISHA DILI NA CHELSEA!!
>>YATAMKA: “NI REKODI KWA KLABU!”
>>MOURINHO AMJIBU WENGER: “HATUOGOPI KAMA ATAFANYA VYEMA HUKO!!
Manchester United Jana Usiku walithibitisha kufikia Makubaliano na Chelsea ili kumnunua Kiungo wa Spain Juan Mata kwa Dau ambalo hawakulitaja ila walisema tu ni ‘Rekodi kwa Klabu’ na Uhamisho huu utakamilika baada kumalizwa kwa upimaji afya wa Mchezaji huyo.
Inakisiwa Dau la kumnunua Mchezaji huyo aliewachezea Mabingwa wa Dunia Spain mara 32 na kufunga Bao 9 ni Pauni Milioni 37 na yeye atakuwa akilipwa Pauni 150,000 kwa Wiki.
Rekodi ya Man United ya kununua Mchezaji kwa Bei ghali iliwekwa Septemba 2008 walipomnunua Dimitar Berbatov kutoka Tottenham kwa Pauni Milioni 30.75.
Mata na Chelsea:
-2011-12: Mechi 54 Goli 12 na kutwaa UEFA CHAMPIONZ LIGI, FA CUP
-2012-13: Mechi 64 Goli 20, na kutwaa Europa Ligi
-2013-14: Mechi 17 Goli 1

Chelsea walimnunua Mata Mwaka 2011 kutoka Valencia kwa Pauni Milioni 23.5.
Jana kwenye Mahojiano na Wanahabari kwa ajili ya Mechi yao ya Wikiendi hii ya FA CUP na Stoke City, Meneja wa Chelsea, Jose Mouringo, aligusia kuhusu Mata na kusema: “Mambo yanakwenda sawa. Tumemruhusu Juan Mata asafiri na kupimwa Afya. Anastahili kuheshimiwa na kucheza na Ofa hii ni sahihi, tumemruhusu ajadiliane. Nilimuuliza Mata Ofa hii ilipokuja kama amefurahiwa na alijibu ndio, nina furaha kuhama. ”
 
Mourinho kuhusu Wenger juu ya Mata
Mourinho aliongeza, na wengi wanadhani ni kumjibu Wenger aliekasirishwa na Mata kwenda Man United, alitamka: "Hii ni nafasi safi kwake. Klabu nyingine kubwa Nchini inamtaka na yeye anataka kubaki Nchini humu, na ingawa Klabu nyingi zinahisi usiwauzie Wachezaji wako wapinzani wako, sisi tuko tofauti. Alikuwa bora kwa Chelsea na Chelsea ilikuwa bora kwake. Hatuogopi kama atafanya vyema huko. Tunataka aende huko na kuwa na furaha!”

0 comments: