Saturday, 25 January 2014

FA CUP: MAN CITY YAICHAPA WITFORD 4-2 ANGALIA MATOKEO YA MECHI ZA LEO

SOMA MECHI KWA MECHI:
MANCHESTER CITY 4 WATFORD 2
FA_CUP_LOGO_NEWHadi Mapumziko, Man City wakicheza kwao Etihad, walikuwa nyuma kwa Bao 2-0, lakini Kipindi Cha Pili Bao za Sergio Aguero na Kolarov ziliwavusha walipoifunga Watford 4-2 na kutinga Raundi ya 5 ya FA CUP.
Bao za Watford zilifungwa na Forestrieri na Troy Deeney.
Nien.
Refa: Kevin Friend

BIRMINGHAM CITY 1 SWANSEA 2
Bao za mbili za Wilfried Bony alietoka Benchi zimewapa Swansea City ushindi wa Bao 2-1 walipoinyuka Ugenini Birmingham City.

Refa: Neil Swarbrick

BOLTON 0 CARDIFF 1
Bao pekee la Straika Frazier Campbell, alietoka Benchi, limewapa ushindo Cardiff City wa Bao 1-0 walipoifunga Bolton Wanderers Bao 1-0.

Refa: Jon Moss

SUNDERLAND 1 KIDDERMINSTER 0
Bao la Dakika ya 5 la Charis Mavrias limewapa Sunderland ushindi wa Bao 1-0 dhidi ya Kidderminister ambayo haichezi Ligi rasmi huko England.

Refa: Lee Mason

WIGAN 2 CRYSTAL PALACE 1
Mabingwa Watetezi wa FA CUP, Wigan, leo wameichapa Crystal Palace Bao 2-1 na kutinga Raundi ya 5 ya FA CUP.
Bao za Wigan zilifungwa na Watson na McClean na Bao la Palace kupachikwa na Wilbraham alietoka Benchi.

Refa: Mike Jones

ROCHDALE 1 SHEFFIELD WEDNESDAY 2
Bao la Oguchi Onyewu limewapa ushindi Sheffield wa 2-1 walipocheza Ugenini huku wakiwa Mtu 10 baada Mfungaji wao wa Bao la kwanza Mattock kutolewa nje kwa Kadi Nyekundu.
Bao la Rochdale lilifungwa na Rose.

Refa: Simon Hooper

PORT VALE 1 BRIGHTON 3
Brighton, waliokuwa Ugenini, waliichapa Port Vale Bao 3-1 kwa Bao za Rohan Ince, March na Obika huku Bao la Vale likifungwa na Robertson.

Refa: Paul Tierney

SOUTHAMPTON 2 YEOVIL 0
Southampton wameifunga Yeovil Bao 2-0 kwa Bao za Do Prado, Penati, na Gallagher.

Refa: Phil Dowd

FA CUP
RATIBA/MATOKEO:
Raundi ya 4
Ijumaa Januari 24
Arsenal 4 Coventry 0
Nottingham Forest 0 Preston 0
Jumamosi Januari 25
[Saa za Bongo]
Bournemouth 0 Liverpool 2
Birmingham 1 Swansea 2
Manchester City 4 Watford 2
Wigan 2 Crystal Palace 1
Rochdale 1 Sheffield Wednesday 2
Southend 0 Hull City 2
Port Vale 1 Brighton 3
Huddersfield 0 Charlton 1
Southampton 2 Yeovil 0
Bolton 0 Cardiff 1
Sunderland 1 Kidderminister 0
[Saa 20:30]
Stevenage v Everton
Jumapili Januari 26
16:00 Sheffield United v Fulham
18:30 Chelsea v Stoke

THE FA CUP WITH BUDWEISER
MSIMU 2013-14
TAREHE ZA RAUNDI:
-RAUNDI YA 3: Jumamosi Januari 4 [KLABU ZA LIGI KUU ENGLAND HUANZA]
-RAUNDI YA 4: Jumamosi Januari 25
-RAUNDI YA 5: Jumamosi Februari 15
-RAUNDI YA 6: Jumamosi Machi 8
-NUSU FAINALI: Jumamosi Aprili 12 & Jumapili Aprili 13
-FAINALI: Jumamosi Mei 17

0 comments: