Saturday, 25 January 2014

CHAN 2014: NIGERIA 4-0 YATINGA NUSU FAINALI KUKUTANA NA GHANA AU CONGO


ROBO FAINALI
RATIBA/MATOKEO:
Jumamosi Januari 25
[Saa za Bongo]
[Cape Town Stadium]
Morocco 3 Nigeria 4 [3-3 baada Dakika 90]
2130 Mali v Zimbabwe

Hii leo huko Cape Town, Nigeria walitoka nyuma kwa Bao 3-0 hadi Haftaimu na kuichapa Morocco 4-3 katika Mechi ya Robo Fainali ya CHAN 2014, ambayo ni michuano ya Mataifa ya Afrika kwa Wachezaji wanaocheza ndani ya Nchi zao, yanayochezwa huko Afrika Kusini.

MAGOLI:
Morocco 3
-Moutaouali Dakika ya 33 & 40
-Iajour 37
Nigeria 4
-Uzochukwu Dakika ya 49
-Ali 56
-Uzoenyi 90
-Ibrahim 111

CHAN2014_LOGOWakiwa nyuma kwa Bao 3-0, Nigeria walipigana na kurudisha Bao 2 na kisha kusawazisha katika Dakika ya 90 kwa Bao la Uzoenyi na Mechi kwenda Dakika 30 za Nyongeza ambapo Aliyu Ibrahim, alietoka Benchi, alifunga Bao la 4 na la ushindi kwa Nigeria katika Dakika ya 111.
Sasa Nigeria wametinga Nusu Fainali na watacheza na Mshindi kati ya Ghana na Congo DR.
VIKOSI:
Morocco: Lamyarghri, El Ouadi, El Hachimi, Karrouchi, Erraki, Abarhoun, Oulhaj, Rafik, Said (Achchakir 58’), Iajour, Moutaouali (El Bahri 76’)
Nigeria: Agbim, Egwuekwe, Esieme, Obanor, Kunle, Ali, Shehu (Umar 113’), Uzochukwu, Ifeanyi (Ibrahim 64’), Uzoenyi, Salami (Imenger 50’)
ROBO FAINALI
[SAA za Bongo]
Jumapili Januari 26
1800 Gabon v Libya [Peter Mokaba Stadium]
2130 Ghana v Congo DR [Free State Stadium]
NUSU FAINALI
Jumatano Januari 29
1800 Mali/Zimbabwe v Gabon/Libya [Free State Stadium]
2130 Ghana/Congo DR v Nigeria [Free State Stadium]
Jumamosi Februari 1
1800 Mshindi wa Tatu [Cape Town Stadium]
2100 Fainali [Cape Town Stadium]

0 comments: