Sunday, 5 January 2014

MAPINDUZI CUP-MIAKA 50: AZAM IPO ROBO FAINALI!ASHANTI NA, MBEYA CITY MGUU MMOJA NJE!!

>>SIMBA v KMKM JUMAPILI!
MABINGWA WATETEZI wa Kombe la Mapinduzi, Azam FC, wametinga Robo Fainali ya Kombe hiliZANZIBAR_STONE_TOWN baada kuifunga Tusker ya Kenya Bao 1-0 Usiku huu huko Amaan Stadium, Zanzibar.
Bao la ushindi kwa Azam FC lilifungwa na Kipre Tchetche.
Azam FC wanaongoza Kundi C wakiwa na Pointi 6 wakifuatiwa na Tusker, wenye Pointi 3, na Ashanti na Spice Stars, ambayo ni Kombaini ya Zanzibar, wakiwa na Pointi 1 kila mmoja kufuatia kutoka Sare ya Bao 1-1 hio leo.

MSIMAMO:
[Kila Timu imecheza Mechi 2]
KUNDI A:
1 URA Pointi 4
2 Chuoni 4
3 Mbeya City 1
4 Clove Stars 1
KUNDI B:
1 KCC Pointi 4
2 Simba 4
3 KMKM 1
4 AFC Leopards 1
KUNDI C:
1 Azam FC Pointi 6
2 Tusker 3
3 Ashanti 1
4 Spice Stars 1
**Robo Fainali  Jumatano Januari 8.
**Nusu Fainali Ijumaa Januari 10
**Fainali Januari 13.

Katika Mechi nyingine za Kundi A zilizochezwa huko Gombani Visiwani Pemba URA ya Uganda iliichapa Clove Stars, Kombaini ya Pemba, Bao 3-1 na Chuoni kuipiga Mbeya City Bao 2-1.
URA na Chuoni ziko juu kwenye Kundi zote zikiwa na Pointi 4 na Mbeya City na Clove Stars wakiwa na Pointi 1 kila mmoja.
Timu mbili za juu kila Kundi zitasonga Robo Fainali na Timu mbili Bora kwenye Nafasi za Tatu toka Makundi hayo matatu zitaungana nao.
RATIBA/MATOKEO:
Jumatano Januari 1
[Amaan Stadium, Zanzibar]
KMKM 2 KCC 3
Simba 1 AFC 0
Alhamisi Januari 2
[Amaan Stadium, Zanzibar]
Ashanti 0 Tusker 1
Spice Stars 0 Azam 2
[Gombani Stadium, Pemba]
URA (Uganda) 2 Chuoni 2
Mbeya City 1 Clove Stars 1
Ijumaa Januari 3
[Amaan Stadium, Zanzibar]
KMKM 0 AFC Leopards 0
Simba 0 KCC 0
Jumamosi Januari 4
[Gombani Stadium, Pemba]
Clove Stars 1 URA 3
Chuoni 2 Mbeya City 1
[Amaan Stadium, Zanzibar]
Ashanti 1 Spice Stars 1
Azam 1 Tusker 0
Jumapili Januari 5
Saa 10 Jioni
KCC v AFC Leopards
Saa 2 Usiku
Simba v KMKM

Related Posts:

0 comments: