Wanahabari Iringa wakiwa na mwenyekiti
wao aliyeachiwa huru Frank Leonard wa nne kushoto baada ya kuachiwa
huru na jeshi la polisi leo
........................................................................
Askari wa jeshi la polisi mkoa wa
Iringa wamemwachia huru mwenyekiti wa chama cha waandishi wa
habari mkoa wa Iringa (IPC) Frank Leonard ambae ni mwandishi wa
magazeti ya serikali mkoani Iringa aliyekamatwa ndani ya chumba cha
mahakama wakati akifuatilia mwenendo wa kesi ya mtuhumiwa wa mauwaji
ya aliyekuwa mwenyekiti wa IPC Marehemu Daudi Mwangosi.Polisi hao wamemwachia huru Leonard baada ya kukosa ukweli wa kesi hiyo waliyotaka kumbambikia kuwa amepiga picha mahakamani wakati mtuhumiwa wa mauwaji hayo ambae ni askari mwenzao akisomewa mashtaka yake.
Hata hivyo mwanahabari huyo ambae hakuwa amewasha kamera yake mahakamani hapo alikuwa ameshika simu yake kabla ya askatri mmoja kusimama na kumkamata ndani ya mahakama wakati kesi hiyo ikiendelea.
0 comments:
Post a Comment