Friday, 17 January 2014

MAKUNDI YA URAIS YAIVUGA NA KUIGAWANYA CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM)

 
Makundi ya Urais wa 2015 yanaendelea kuivuruga CCM baada ya Mwenyekiti wa chama hicho Mkoa wa Singida, Mgana Msindai kuibuka na kusema atamburuta mahakamani Mwenyekiti mwenzake wa Mkoa wa Geita, Joseph Kasheku 'Msukuma' asipomwomba radhi kwa kumchafua kwa kumwita mpuuzi.Hata hivyo, Kasheku amesema Msindai anaweza kwenda mahakamani huku akisisitiza kwamba hawezi kumwomba radhi kwa kuwa anaamini kwamba alichofanya ni kinyume cha taratibu za chama na vikao.
Juzi, Kasheku alimponda Msindai mbele ya waandishi wa habari kwa kitendo chake cha kusema kuwa wenyeviti wa CCM wa mikoa yote ya Tanzania wanamuunga mkono, Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa katika safari yake ya urais wa 2015 wakati wa sherehe ya mwaka mpya huko Monduli, Arusha.
Msindai alisema jana kuwa amemtaka Kasheku aitishe mkutano wa waandishi wa habari na kumwomba radhi. "Asipofanya hivyo ndani ya siku saba nitampeleka mahakamani," alisema Msindai.
Msindai pia alikanusha kuwa aliwekwa kitimoto katika mkutano wa wenyeviti wa CCM wa mikoa uliofanyika Zanzibar.
Msindai aliyekuwa Mbunge wa Iramba Mashariki kwa miaka 15, alikiri kuwa alialikwa pamoja na wenyeviti wenzake sita katika sherehe ya mwaka mpya iliyoandaliwa na Lowassa huko Monduli.
Katika sherehe hizo, Lowassa alitangaza kuwa ameanza safari ya matumaini, kauli ambayo wachambuzi wa masuala ya kisiasa waliitafsiri kama tangazo la kuwania urais mwaka 2015.
Soma zaidi...

Related Posts:

0 comments: