Saturday, 11 January 2014

LIGI KUU ENGLAND: MECHI ZA WIKIENDI


>>FUNGUA DIMBA JUMAMOSI: HULL v CHELSEA!
>>FUNGA DIMBA JUMAMOSI: MAN UNITED v SWANSEA!BPL2013LOGO
SOMA ZAIDI:
+++++++++++++++++++++++
RATIBA:
Jumamosi Januari 11
[Saa za Bongo]
1545 Hull v Chelsea
1800 Cardiff v West Ham
1800 Everton v Norwich
1800 Fulham v Sunderland
1800 Southampton v West Brom
1800 Tottenham v Crystal Palace
2030 Man United v Swansea
+++++++++++++++++++++++
HULL CITY v CHELSEA
-KC Stadium
Hull City wameshinda Mechi moja tu ya Ligi katika 7 na hiyo ni kipondo cha Bao 6-0  walipoitwanga Fulham na wanakutana na Chelsea ambayo Magoli yao hufungwa na Viungo, si Mastraika, huku Oscar, Eden Hazard na Willian, wakiwa hatari ingawa watamkosa Majeruhi Frank Lampard ambae ni Kiungo wao Veterani na mahiri kwa Mabao.
CARDIFF CITY v WEST HAM UNITED
-Cardiff City Stadium
Hii ni Mechi ya kwanza ya Ligi kwa Lejendari wa Manchester United, Ole Gunnar Solskjaer, tangu atwae Umeneja wa Cardiff City Wiki iliyopita ambapo katika Mechi yake ya kwanza kabisa waliifunga Newcastle 2-0 kwenye FA CUP.
Cardiff wanakutana na West Ham ambayo iko mashakani kwa kushinda Mechi moja tu katika 10 na katika Mechi zao mbili zilizopita walibandikwa 5-0 na Nottingham Forest kwenye FA CUP  na kuwashwa 6-0 na Man City kwenye Capital One Cup.
Balaa zaidi kwao ni kuwa wanatinga Mechi hii bila Nahodha wao mzoefu Kevin Nolan ambae yuko Kifungoni kwa Kadi Nyekundu.
EVERTON V NORWICH CITY
-Goodison Park
Norwich hawajashinda katika Mechi 5 za Ligi lakini hawatafurahia kukutana na Everton ingawa Everton haijawafunga tangu 2005.
FULHAM V SUNDERLAND
-Craven Cottage
Hii ni Mechi ya ‘Piga Ua’ kwani Sunderland wako mkiani na Fulham wanahitaji ushindi ili wawe Pointi 5 toka Timu 3 za mkiani.
SOUTHAMPTON V WEST BROMWITH ALBION
-St Mary’s
Timu hizi mbili zimeshinda Mechi 2 tu kati ya Mechi 19 za Ligi walizocheza Msimu huu.
West Brom watakuwa chini ya Meneja wa muda, Keith Downing, ambae pia ni Kocha Msaidizi na ambae amewasaidia kutofungwa katika Mechi 4 za Ligi akikaimu Nafasi hiyo, kwa mara ya mwisho baada kuteuliwa Meneja mpya Pepe Mel kutoka Spain
TOTTENHAM V CRYSTAL PALACE
-White Hart Lane
Tangu Tim Sherwood achukue Umeneja na kumrudisha Uwanjani Emmanuel Adebayor, Tottenham wamekuwa moto kwa kunyakua Pointi 10 katika Mechi za Ligi 4 huku Adebayor akipiga Bao 3.
Katika Mechi ya kwanza ya Ligi Msimu huu, Penati ya Roberto Soldado iliwapa ushindi Tottenham dhidi ya Cardiff.
MANCHESTER UNITED V SWANSEA CITY
-Old Trafford
Hii ni mara ya pili kwa Man United kukutana na Swansea City Uwanjani Old Trafford ndani ya Siku 6.
Swansea walishinda kwa mara ya kwanza kabisa walipoifunga Man United 2-1 kwenye Kombe la FA Jumapili iliyopita lakini pengine Meneja wa Swansea, Michael Laudrup, angependelea Pointi zaidi baada ya kutoshinda katika Mechi 6 za Ligi zilizopita.
Lakini wanakutana na Man United ambayo haijashinda Mechi yeyote kwa Mwaka 2014 baada kuchapwa Mechi zao zote 3 Mwaka huu na ambao wanatarajiwa kuingia na moto mkali.
NEWCASTLE UNITED V MANCHESTER CITY
-St James’ Park
Tangu Manuel Pellegrini atue Manchester City ndio kwanza wameshinda Mechi mbili za Ugenini hivi Juzi na inaelekea wanaweza kushinda Mechi hii kwa vile Newcastle hawajaifunga City tangu 2005.
STOKE CITY V LIVERPOOL
-Britannia Stadium
Liverpool wanaweza kuimarika kwa kurudi kilingeni kwa Straika Daniel Sturridge lakini wana tatizo kubwa la Mechi za Ugenini ambapo wameambua Pointi 4 tu kati Mechi zao 6 zilizopita.
Stoke, ambao walifungwa kwa Bao la Sturridge huko Anfield Mwezi Agosti, hawajafungwa katika Mechi 7 za Ligi za Nyumbani na hawajafungwa na Liverpool wakiwa kwao Britannia kwenye Ligi Kuu kwa kushinda Mechi 3 na Sare 2.
ASTON VILLA V ARSENAL
-Villa Park
Hii ni nafasi murua kwa Arsene Wenger kulipiza kisasi kwa kubamizwa Bao 3-1 kwao Emirates Siku ya ufunguzi wa Msimu mpya wa Ligi Mwezi Agosti.
Straika wa Aston Villa Christian Benteke alipiga Bao 2 katika kipigo hicho cha 3-1 lakini hajafunga Bao katika Mechi 12 za Ligi na hili linachangia Villa kufunga Bao 7 tu katika Mechi zao 10 za Nyumbani.
RATIBA:
[Saa za Bongo]
Jumapili Januari 12
1705 Newcastle v Man City
1910 Stoke v Liverpool
Jumatatu Januari 13
2300 Aston Villa v Arsenal
MSIMAMO:
NA
TIMU
P
GD
PTS
1
Arsenal
20
21
45
2
Man City
20
34
44
3
Chelsea
20
19
43
4
Liverpool
20
23
39
5
Everton
20
13
38
6
Tottenham
20
-1
37
7
Man Utd
20
9
34
8
Newcastle
20
4
33
9
Southampton
20
3
27
10
Hull
20
-3
23
11
Aston Villa
20
-6
23
12
Stoke
20
-11
22
13
Swansea
20
-2
21
14
West Brom
20
-4
21
15
Norwich
20
-16
20
16
Fulham
20
-21
19
17
Cardiff
20
-17
18
18
Crystal Palace
20
-16
17
19
West Ham
20
-11
15
20
Sunderland
20
-18
14

Related Posts:

0 comments: