>>LEO PIA: ROVERS v CITY, EVERTON v QPR!!
>>JUMAPILI: MAN UNITED v SWANSEA, DERBY v CHELSEA, LIVERPOOL v OLDHAM!!
ARSENE
WENGER amewaonya Mastaa wake kutoteleza wakati Tottenham leo
watakapotua Uwaja wa Emirates kucheza Mechi ya Raundi ya Tatu ya FA CUP.
Msimu uliopita, Arsenal ilibwagwa nje ya
Kombe hili kwenye Raundi ya Tano na Timu ya Daraja la chini, la
Championship, Blackburn Rovers.
Huo ulikuwa ni mfululizo wa kubolonga kwa Arsenal na kushindwa kutwaa Kombe lolote tangu Mwaka 2005.
Lakini safari hii, Wenger anaamini Timu yake, ambayo ndio Vinara wa Ligi Kuu England, wanajiamini zaidi na wana ari ya ushindi.
Wenger amesema: “Nimebahatika kushinda
FA CUP mara 4 na hii inamaanisha najitahidi kila mara kushinda. Nina nia
kubwa kulitwaa tena ingawa ni muda mrefu sasa.”
Aliongeza: “Ukweli, nakumbuka Mwaka Jana
tulitolewa tuko Nyumbani na Blackburn, na hilo sio jambo zuri kwetu na
lazima tujitahidi kupita. Hatujatwaa Mataji muda mrefu, na hii ni fursa
tunayotaka kuikamata!”
Mara ya mwisho kwa Arsenal kutwaa FA CUP
ni Mwaka 2005 walipoifunga Manchester United na hilo ndio Kombe lao la
mwisho kabisa kutwaa tangu wakati huo.
Ingawa Wenger ana matumaini makubwa
lakini hii ni Dabi ya London na lolote linaweza kutokea hasa kwa vile,
Tottenham, chini ya Meneja mpya, Tim Sherwood, wapo na morali kubwa hasa
baada ya kuwafunga Mabingwa wa England Man United Bao 2-1 Siku ya Mwaka
mpya kwenye Mechi ya Ligi.
Ukiondoa Mechi hii ya Arsenal v
Tottenham, Raundi ya Tatu ya FA CUP haina Mechi zinazotarajiwa kuwa za
vuta nikuvute na Liverpool, Aston Villa na Sunderland zote zinacheza na
Timu za Daraja la Tatu, Oldham Athletic, Sheffield United na Carlisle
United.
Chelsea wao watakuwa Ugenini kucheza na
Derby County ambayo ipo Daraja la chini tu ya Ligi Kuu England,
Championship, wakiongozwa na Meneja wa zamani wa England, Steve
McClaren.
Man City nao pia wako Ugenini kucheza na Blackburn Rovers.
Mechi ambayo ni kushangaza ni ile kati
ya Timu ambayo haipo kwenye Ligi, Macclesfield Town, watakaokuwa
Nyumbani kuikaribisha Sheffield Wednesday, inayocheza Daraja la
Championship, wakiwa wapo Nafasi 63 juu ya Macclesfield Town katika
Mfumo wa Ligi za England.
RATIBA
RAUNDI ya TATU
Jumamosi Januari 4
[Saa za Bongo]
1545 Blackburn v Manchester City
[Zote zinazofuata Saa 1800]
Bournemouth v Burton
Ipswich v Preston
Grimsby v Huddersfield
Brighton v Reading
Everton v QPR
Bolton v Blackpool
Macclesfield v Sheffield Wednesday
Aston Villa v Sheffield United
Norwich v Fulham
Charlton v Oxford United
Wigan v MK Dons
Rochdale v Leeds
Newcastle v Cardiff
Southampton v Burnley
Stoke v Leicester
Doncaster v Stevenage
Kidderminster v Peterborough
West Brom v Crystal Palace
Middlesbrough v Hull
Southend v Millwall
Bristol City v Watford
Yeovil v Leyton Orient
Barnsley v Hartlepool au Coventry
2015 Arsenal v Tottenham
Jumapili Januari 5
1500 Nottingham Forest v West Ham
1700 Sunderland v Carlisle
1715 Derby v Chelsea
1800 Liverpool v Oldham
1800 Port Vale v Plymouth
1930 Manchester United v Swansea
THE FA CUP WITH BUDWEISER
MSIMU 2013-14
TAREHE ZA RAUNDI:
-RAUNDI YA 3: Jumamosi Januari 4 [KLABU ZA LIGI KUU ENGLAND HUANZA]
-RAUNDI YA 4: Jumamosi Januari 25
-RAUNDI YA 5: Jumamosi Februari 15
-RAUNDI YA 6: Jumamosi Machi 8
-NUSU FAINALI: Jumamosi Aprili 12 & Jumapili Aprili 13
-FAINALI: Jumamosi Mei 17
0 comments:
Post a Comment