Saturday, 4 January 2014

ANGALIA MATOKEO NA RATIBA MAPINDUZI CUP-MIAKA 50: SIMBA, KCC SARE!

>>KMKM, AFC LEOPARDS 0-0!
Mechi zote za Kundi B za Mashindano ya Kombe la Mapinduzi, ambayo ni moja ya ShereheZANZIBAR_STONE_TOWNmaalum za kuadhimisha Miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar, zilizochezwa hii leo huko Amaan Stadium, Zanzibar zilimalizika kwa Sare.
Katika Mechi ya Kwanza, KMKM ilitoka 0-0 na AFC Leopards ya Kenya na Simba pia kutoka 0-0 na KCC ya Uganda.
 
Makundi:
-KUNDI A: Mbeya City, Clove Stars [Kombaini ya Pemba], Chuoni, URA (Uganda)
-KUNDI B: Simba, KMKM, AFC Leopards (Kenya), KCC (Uganda)
-KUNDI C: Azam, Tusker (Kenya), Ashanti, Spice Stars [Kombaini ya Zanzibar]
**Robo Fainali  Jumatano Januari 8.
**Nusu Fainali Ijumaa Januari 10
**Fainali Januari 13.
Baada ya Mechi mbili, KCC na Simba ziko kileleni zikiwa na Pointi 4 kila moja na kufuatia KMKM na AFC Leopards zenye Pointi moja kila mmoja.
Mechi za mwisho kwa Kundi hili ni Januari 5 ambapo KCC watacheza na AFC Leopards na KMKM kuikwaa Simba.
Jumamosi zipo Mechi 4, mbili kuchezwa Gombani Stadium huko Pemba na mbili huko Anaan Stadium Zanzibar.
RATIBA/MATOKEO:
Jumatano Januari 1
[Amaan Stadium, Zanzibar]
KMKM 2 KCC 3
Simba 1 AFC 0
Alhamisi Januari 2
[Amaan Stadium, Zanzibar]
Ashanti 0 Tusker 1
Spice Stars 0 Azam 2
[Gombani Stadium, Pemba]
URA (Uganda) 2 Chuoni 2
Mbeya City 1 Clove Stars 1
Ijumaa Januari 3
[Amaan Stadium, Zanzibar]
KMKM 0 AFC Leopards 0
Simba KCC
Jumamosi Januari 4
[Gombani Stadium, Pemba]
Saa 8 Mchana
Clove Stars v URA
Saa 10 Jioni
Chuoni v Mbeya City
[Amaan Stadium, Zanzibar]
Saa 10 Jioni
Ashanti v Spice Stars
Saa 2 Usiku
Azam v Tusker
Jumapili Januari 5
Saa 10 Jioni
KCC v AFC Leopards
Saa 2 Usiku
Simba v KMKM

0 comments: