Sunday, 19 January 2014

CHELSEA YAICHAPA MANCHESTER UNITED 3-1ETO'O APIGA BAO ZOTE TATU


>>WADAU WADAI KILICHOBAKI SASA NI KUPIGANIA 4 BORA TU!
>>HETITRIKI YA GWIJI WA CAMEROUN, ETO’O, YAIUA UNITED!
MATOKEO
Jumapili Januari 19
Swansea 1 Tottenham 3
Chelsea 3 Man United 1

Alikuwa ni Samuel Eto'o aliyeifungia Chelsea magoli yote matatu huku lile la Man United likifungwa na Javier Hernandez


ETOO_IN_CHELSEA2MABINGWA Manchester United walitawala Kipindi cha Kwanza na kujikuta wako nyuma kwa Bao 2-0 dhidi ya Chelsea, Bao zote zikifungwa na Gwiji wa Cameroun Samuel Eto’o, kwenye Mechi ya Ligi Kuu England iliyochezwa Stamford Bridge waliyomaliza kwa kipigo cha Bao 3-1 ambacho kwa Wadau wao huenda kimehakikisha kwamba hawawezi tena kutetea Taji lao kwani sasa wako Pointi 14 nyuma ya Vinara Arsenal huku zimebaki Mechi 16.
Pengine kilichobaki kwao sasa ni kuwania kumaliza ndani ya 4 bora ili wafuzu kucheza UEFA CHAMPIONZ LIGI Msimu ujao kwani wapo Pointi 6 tu nyuma ya Nafasi hiyo ya 4.
Chelsea walipata Bao lao la kwanza katika Dakika ya 17, bila kutegemewa kwani Man United ndio waliokuwa juu kimchezo, baada ya uzembe wa kutomkaba Samuel Eto'o ambae alipokea Mpira wa kurushwa na kumhadaa kirahisi Phil Jones kisha kupiga Shuti la Mita 20 na kumbabatiza Mchael Carrick na kumpoteza Kipa De Gea.
Bao la Pili lilifungwa kwenye Dakika ya 45 na Eto’o kufuatia ulinzi duni baada Kona kupigwa na kuokolewa na Mpira kumkuta Ramires aliempasia Cahill aliemsogezea Eto’o na kupachika kilaini.
Bao la 3 lilipigwa tena na Eto’o, ni Hetitriki kwake, kufuatia Kona ya Dakika ya 49 iliyounganishwa na Cahill na kuokolewa na De Gea na kutua miguuni mwa Eto’o ambae alimalizia kilaini kwa mara nyingine.
Javier Hernandez ‘Chicharito’ aliifungia Bao lao pekee Man United katika Dakika ya 78 kufuatia kazi njema ya Danny Welbeck kumfikia Phil Jones ambae shuti lake lilionekana kutokuwa na madhara hadi alipochomoza Chicharito.
Man United walimaliza Mechi hii Mtu 10 baada Nahodha wao Nemanja Vidic kupewa Kadi Nyekundu kwa Rafu mbaya kwa Eden Hazard.
VIKOSI:
CHELSEA: Cech, Ivanovic, Cahill, Terry, Azpilicueta, Ramires, Luiz, Willian, Oscar, Hazard, Eto'o
Akiba: Cole, Lampard, Torres, Mata, Mikel, Matic, Schwarzer.
MAN UNITED: De Gea, Rafael Da Silva, Evans, Vidic, Evra, Jones, Carrick, Valencia, Januzaj, Young, Welbeck
Akiba: Giggs, Smalling, Lindegaard, Hernandez, Cleverley, Fletcher, Kagawa.
REFA: PHIL DOWD
MSIMAMO:
NA TIMU P GD PTS
1 Arsenal 22 24 51
2 Man City 22 38 50
3 Chelsea 22 23 49
4 Liverpool 22 25 43
5 Tottenham 22 3 43
6 Everton 21 15 41
7 Man Utd 22 9 37
8 Newcastle 22 4 36
9 Southampton 22 4 31
10 Aston Villa 22 -7 24
11 Hull 22 -6 23
12 Norwich 22 -17 23
13 Stoke 22 -14 22
14 West Brom 21 -5 21
15 Swansea 22 -6 21
16 Crystal Palace 22 -17 20
17 Fulham 22 -26 19
18 West Ham 22 -11 18
19 Sunderland 22 -15 18
20 Cardiff 22 -21 18
RATIBA:
[Saa za Bongo]
Jumatatu Januari 20
2300 West Brom v Everton
Jumanne Januari 28
2245 Man Utd v Cardiff
2245 Norwich v Newcastle
2245 Southampton v Arsenal
2245 Swansea v Fulham
2300 Crystal Palace v Hull
2300 Liverpool v Everton
Jumatano Januari 29
2245 Aston Villa v West Brom
2245 Chelsea v West Ham
2245 Sunderland v Stoke
2245 Tottenham v Man City

Related Posts:

0 comments: