Milipuko miwili mikubwa imetokea nchini Nigeria katika mji wa Jos.
Milipuko hiyo imetokea katika soko
ambalo lina shughuli nyingi na ambalo lilikuwa na msongamano wa watu
eneo la Kati mwa Nigeria.Mwandishi wa BBC Ishaq Khalid aliye mjini humo anasema kuwa kuna hofu ya watu wengi kujeruhiwa hasa kwa kuwa soko hilo lilikuwa na idadi kubwa ya watu.
Haijulikani kilichosababisha milipuko hiyo mjini Jos, mji ambao umeshuhudia mashambulizi makali kati ya wakristo na waisilamu.
Kundi la Boko Haram, pia limekuwa likifanya mashambulizi katika mji huo.CHANZO BBC,
0 comments:
Post a Comment