Tuesday, 20 May 2014

BARCELONA YAACHANA NA PINTO, MESSI APOTEZA RAFIKI

 


Lionel Messi atampoteza rafiki yake José Manuel Pinto baada ya Barcelona kusema wazi haimhitaji.

Uongozi wa Barcelona umesema hautamuongezea Pinto mkataba mpya, hivyo yuko huru kuondoka.
Pinto amekuwa rafiki wa karibu wa Messi licha ya kwamba mshambuliaji huyo amekuwa akionekana mgumu kuanzishaurafiki na wageni.
Lakini tokea Pinto alipotua msimu wa 2008-09, kipa huyo alikuwa karibu sana na Messi.
Hata kabla ya Messi kusaini mkataba mpya, Messi alijaribu kutaka kujua kama Pinto atapewa mkataba mpya.

0 comments: