>> SHERIA BAO LA UGENINI HUTUMIKA TU BAADA DAKIKA 120!!
CAPITAL ONE CUP
RATIBA/MATOKEO:
NUSU FAINALI
Jumanne Januari 7
Sunderland 2 Man United 1
Jumatano Januari 8
Man City 6 West Ham 0
Marudiano
[Saa 4 Dakika 45 Usiku]
Jumanne Januari 21
West Ham v Man City
Jumatano Januari 22
Man United v Sunderland
ZIFUATAZO NI TATTHMINI ZA MECHI HIZI:
WEST HAM v MANCHESTER CITY
Manchester City watatinga Upton Park
wakiwa mguu mmoja ndani ya Fainali baada kuinyuka West Ham Bao 6-0
katika Mechi ya Kwanza ingawa Meneja wao Manuel Pellegrini amesisitiza
mambo bado.
City inatarajiwa kupumzisha Wachezaji wao kadhaa na kuwapa namba wale wasiokuwa na namba za kudumu.
Hali kadhalika, Sam Allardyce, Meneja wa
West Ham, licha ya kutokiri hadharani kwamba hawana nafasi ya kwenda
Fainali, anategemewa pia kupumzisha Wachezaji wake kadhaa huku jicho
likiwa kwenye Mechi yao ngumu ijayo ya Ligi Kuu England huko Stamford
Bridge dhidi ya Chelsea.
Lakini West Ham itawakaribisha tena
Nahodha wao Kevin Nolan na Sentahafu James Tomkins ambao walikuwa
Kifungoni na pia kuwachezesha Straika Andy Carroll, ambae ndio kwanza
amerudi toka Majeruhi ya muda mrefu, pamoja na Kiungo Ravel Morrison.
Vile vile, West Ham inatarajiwa kumchezesha Fowadi wao Ricardo Vaz Te ambae alikuwa nje kwa Miezi Mitatu akijiuguza Bega lake.
VIKOSI VINATARAJIWA KUTOKA:
West Ham: Jaaskelainen,
Adrian, O'Brien, Johnson, Tomkins, Collins, Rat, Demel, McCartney,
Diarra, Noble, Collison, Jarvis, Taylor, J Cole, Diame, Nolan, Morrison,
Vaz Te, Maiga, C Cole, Carroll.
Manchester City:
Pantilimon, Hart, Richards, Zabaleta, Huws, Nastasic, Lescott, Kompany,
Demichelis, Boyata, Clichy, Kolarov, Milner, Navas, Silva, Toure,
Fernandinho, Garcia, Rodwell, Lopes, Aguero, Jovetic, Dzeko, Negredo
REFA: Christopher Foy
MAN UNITED v SUNDERLAND
Inaelekea Wayne Rooney na Robin van
Persie wataendelea kukosa Mechi hii ya Timu yao Man United licha ya
Rooney kuanza Mazoezi Alhamisi iliyopita, wote wakitokea kujitibu
maumivu yao.
Pia, Man United watamkosa Nahodha wao
Nemanja Vidic ambae ndio anaanza Kifungo chake cha Mechi 3 baada kupewa
Kadi Nyekundu huko Stamford Bridge Jumapili walipofungwa 3-1 na Chelsea
kwenye Mechi ya Ligi.
Baada kutupwa nje kwenye FA CUP na
Swansea City mwanzoni mwa Mwezi huu Januari na pia kuachwa mbali kwenye
Ligi wakiwa Pointi 14 nyuma ya Vinara Arsenal, kwa Man United, Kombe
hili, pengine pamoja na UEFA CHAMPIONZ LIGI, ndio njia pekee za kutwaa
na kuongeza Mataji Msimu huu ukiihesabu Ngao ya Jamii waliyotwaa
mwanzoni mwa Msimu.
Lakini hii itakuwa Mechi ngumu kwa
Mabingwa hao wa England ambao wanatakiwa kupindua kipigo cha Bao 2-1
walichopewa na Sunderland ambayo tangu impate Meneja mpya Gus Poyet
imejiimarisha kwa kutofungwa katika Mechi 4 na Juzi ilitoka nyuma kwa
Bao 2-0 na kupata Sare ya Bao 2-2 na Southampton.
Kwenye Mechi hii, tegemeo kubwa la
Sunderland ni Winga Adam Johnson, Mchezaji wa Mkopo toka Liverpool Fabio
Borini na Kiungo mchapakazi, Ki Sung-Yeung.
Katika ushindi huo wa Bao 2-1,
Sunderland walipata Bao zao kwa Veterani wa Man United Ryan Giggs
kujifunga wenyewe Bao la kwanza na Penati ya Fabio Borini
iliyolalamikiwa sana na Meneja wa Man United, David Moyes, kiasi cha
kumtitia matani na FA na kupigwa Faini Pauni 8,000.
Ili kutinga Fainali, Man United
wanahitaji ushindi wa Bao 1-0 lakini Matokeo hayo kwanza yatalazimisha
Mechi kwenda Dakika 30 za nyongeza kwani Jumla ya Mabao itakuwa 2-2 na
hadi hatua hiyo Bao la Ugenini halihesabiki mawili.
Lakini ikiwa Matokeo yatabaki 1-0 kwa
Man United hadi mwisho wa Dakika 120, hapo ndipo Sheria ya Bao la
Ugenini kuhesabika mawili itatumika na Man United kutinga Fainali.
VIKOSI VINATARAJIWA:
Man United: De Gea; Rafael, Smalling, Evans, Evra; Valencia, Carrick, Fletcher, Januzaj; Hernandez, Welbeck
Sunderland: Mannone; Bardsley, Alonso, Brown, O'Shea; Cattermole, Larsson, Ki, Johnson; Borini, Altidore
REFA: Lee Mason
DONDOO MUHIMU:
-KLABU 92 za BPL [Klabu
20] na Ligi za Madaraja Matatu ya chini [Championship, Ligi 1 na 2,
Jumla Klabu 24 kila Ligi] hushiriki Raundi 7 za Mashindano.
-NUSU FAINALI huchezwa kwa Mtindo wa Mtoano wa Nyumbani na Ugenini.
-KLABU ZA BPL HUANZA
kushiriki Raundi ya Pili lakini zile ambazo zinacheza Mashindano ya UEFA
ya CHAMPIONZ LIGI na EUROPA LIGI huanza kucheza Raundi ya Tatu.
-FAINALI ITACHEZWA TAREHE 2 MACHI 2014 Uwanja wa Wembley na Bingwa hushiriki UEFA EUROPA LIGI Msimu unaofuata.
-MFUMO:
Raundi ya 1: Wiki ya kuanzia Agosti 5
Raundi ya 2: Wiki ya kuanzia Agosti 26
Raundi ya 3: Wiki ya kuanzia Septemba 23
Raundi ya 4: Wiki ya kuanzia Oktoba 28
Raundi ya 5: Wiki ya kuanzia Desemba 16
Nusu Fainali-Mechi ya Kwanza: Wiki ya kuanzia Januari 6
Nusu Fainali-Marudiano: Wiki ya kuanzia Januari 20
Fainali: Jumapili 2 Machi 2014
0 comments:
Post a Comment