Breaking News….Basi la Mtei Express laua watoto watatu wa familia moja mkoani Singida
Basi
la Kampuni ya Mtei Express liliokuwa likifanya Safari zake Singida –
Arusha lenye namba za usajili T742 ACU limeua watoto watatu wa familia
moja waliokuwa wamepakizwa kwenye pikipiki na baba yao mzazi ambaye yuko
mahututi baada ya kupasuka kichwa, ajali hiyo imetokea kwenye kijiji
cha Kititimo mkoani Singida.
Wananchi wenye hasira kali wameamua kulipiga moto basi hilo pamoja na mizigo yake huku abiria wake wakiwa wamesalimika.
Hii
ni taarifa fupi iliyotufikia hivi punde kutoka kwa mwakilishi wa MOblog
Nathaniel Limu wa mkoani Singida aliyepo eneo la tukio. Pichani ni mmoja ya mabasi ya kampuni ya Mtei Express.
Habari zaidi na picha ni hapo baadae.
0 comments:
Post a Comment