Picha ya ajabu inaonyesha wabunge wakishikana mashati wakati wa mjadala huo na wa bajeti ya serikali.
.Bingwa wa zamani wa masumbwi uzito wa juu duniani ashuhudia ngumi zikipigwa kati ya wabunge
.Ni Vitaly Klitschko, wengi wakaa mbali naye kwenye malumbano ndani ya ukumbi wa bunge huko Kiev
Na Damas Makangale, MOblog kwa Msaada wa Mtandao
WAKATI
huku nyumbani Tanzania, viongozi wa bunge wamezoea kuita askari wa
bunge kwa msaada wa kuwatoa baadhi ya wabunge wenye misimamo tofauti na
kiti, huko kwa wenzetu ni ngumi tu kupigwa kama wabunge hawaelewani
katika miswada mbalimbali inayojadiliwa bungeni.
Hayo
yametokea tena nchini Ukraine baada ya wabunge wa bunge la nchi hiyo
kuamua kuzichapa kavu kavu kwa kutumia ngumi, vichwa na mateke na
kupelekea mmoja wa watunga sheria hao kupasuka kati kati ya paji la uso.
Demokrasia ina njia mbalimbali za kuonyesha yenyewe …
Katika
nchi ya Uingereza bunge lao kubwa la Westminster, ambalo ni mama wa
mabunge yote mawili wanatumia njia ya kama kuzomea “yay au baaaa”
kushawishi au kupinga hoja.
Lakini
katika nchi ya Ukraine ni vigumu spika au naibu spika na wabunge
wenyewe kukwepa makonde ni jambo lililozoeleka wakati wowote panapokuwa
na tofauti juu ya upigaji kura katika miswada mbalimbali.
Lakini
wabunge hao wakipambana wana hakikisha wanakuwa mbali na mbunge mwenzao
ambaye ni bingwa wa zamani wa uzito wa juu Vitaly Klitscho ambaye kwa
hakika akitaka kuzipiga kavu kavu watapasuka wengi duru za siasa
zinasema kutoka katika jiji la Kiev.
Wachambuzi
wa mambo na hasa siasa za Kiev wanasema kwamba si mara ya kwamza kwa
viongozi wa Ukraine kuzichapa kavu kavu ndani ya ukumbi wa bunge wengine
wanadiriki kusema ni utamaduni wao.
Mmoja ya mbunge akibubunjika damu.
Vitali Klitschko kiongozi wa chama UDAR chenye ushawishi mkubwa ndani ya ukumbi wa bunge.
Tofauti
ziliibuka pale serikali kwa mshangao wa wapinzani ilipokuja na muswada
wa sheria kali za kupiga marufuku maandamano ya mitaani baada ya kuingia
mikataba kadhaa ya biashara na umoja wa ulaya (EU).
Kambi
ya upinzania bungeni ilikataa kata kata na muswada huo na ndipo
machafuko yalipoanza na baadhi ya mawaziri na wabunge wa chama
kinachotawala kuchapwa mako
0 comments:
Post a Comment