Mradi wa kuongezeka idadi ya mashabiki
katika uwanja wa Manchester City kutoka mashabiki elfu arubaini na nane
hadi elfu sitini na mbili umeidhinishwa.
Klabu hiyo inayoshiriki ligi kuu ya Premier nchini England, itajenga maeneo zaidi ya mashabiki katika uwanja huo.
Mradi huu utajumuisha ujenzi wa maeneo mawili yatakayokuwa na mashambiki elfu nane zaidi.
Ujenzi huo utaifanya uwanja huo wa
Etihad kuwa wa pili kwa ukumbwa nchini Uingereza baada ya uwanja wa
Manchester United wa Old Trafford.
Madiwani wa baraza la jiji la
Manchester, waliidhinisha mradi huo, ambao unatarajiwa kukamilika katika
kipindi cha miaka miwili ijayo.
Manchester City ilihamia uwanja huo mwaka wa 2003.
Awali Uwanja huo ulikuwa na idadi ya
kuchukua mashabiki elfu thelathini na nane, wakati ilipojengwa mwaka wa
2002, kwa matumizi ya michezo ya Jumuiya ya madola.
0 comments:
Post a Comment